Mazungumzo: Ryan Giggs (pichani akiwa na mke wake Stacey mjini Manchester) alikuwa Uholanzi kukutana na Louis van Gaal.
RYAN
Giggs leo mchana alikuwa nchini Uholanzi kwa ajili ya kufanya
mazungumzo na kocha mtarajiwa wa Manchester United, Louis van Gaal.
Kocha
huyo wa muda wa Man United alitakiwa kukutana na Mholanzi huyo mjini
Noordwijk, karibu na Hoteli ambayo timu ya Uholanzi inafanya mazoezi, na
wawili hao walitakiwa kukutana ili kujadili hatima ya baadaye ya Man
United.
Giggs mwenye miaka 40 alionekana akitoka katika hoteli ya Van Oranje
mchana wa leo. Mkurugenzi mkuu wa Man United, Ed Woodward alitakiwa pia kuwepo katika kikao hicho.
0 comments:
Post a Comment