Thursday, May 1, 2014



KOCHA wa Borrusia Dortmund, Jurgen Klopp amesisitiza kuwa Bayern Munich bado ni klabu bora kuliko zote duniani licha ya kutupwa nje hatua ya nusu fainali ya UEFA na Real Madrid.
The Bavarians ambao waliwafunga Dortmund katika fainali ya UEFA mwaka jana uwanja wa Wembley, wameshindwa kutetea ubingwa wao baada ya kupoteza mechi mbili kwa wastani wa mabao 5-0 na Los Blancos (Real Madrid), kufuatia kufungwa mabao 4-0 katika mchezo wa marudiano Allianz Arena.
Klopp amejenga hoja yake kuwa japokuwa Madrid wamedhihirisha kuwa Bayern wanafungika, lakini bado vijana wa Pep Guardiola wanabaki kuwa klabu ya kwanza kwa ubora kwenye sayari hii ya tatu, (dunia).
“Bayern hawakulinda vizuri eneo leo dhidi ya Real Madrid. Kwa upande wangu bado ndio klabu bora duniani, lakini wanaweza kufungika”. Klopp amewaambia waandishi wa habari leo hii.
Klopp kwa sasa atamtumia mshambuliaji wake, Mpoland, Robert Lewandowski katika mechi tatu kabla ya kujiunga na Bayern kufuatia mkataba wake na Dortmund kumalizika majira ya kiangazi mwaka huu.
Klopp aliongeza kuwa : “Lewandowski amekuwa mashambuliaji wa aina yake kwetu na tumefurahi kuwa naye muda wote. Natumaini atafanya kazi nzuri katika mechi tatu alizosaliwa nazo”.
Dortmaund wanakutana na Hoffenheim katika mchezo wao wa mwisho nyumbani Signal Iduna Park kabla ya kusafiri katika mechi moja ya mwisho ya Bundesliga na kumalizia na fainali ya DFB Pokal dhidi ya Bayern Munich ambayo itachezwa katika uwanja wa Olympiastadion.
Klopp,amekataa kuzungumzia sana mchezo wa wikiendi.
“Ni mchezo wetu wa mwisho nyumbani msimu huu kabla ya kwenda Berlin mara mbili na tunahitaji kuufurahia kwa njia sahihi. Alieleza kocha huyo mwenye miaka 45.
“Roberto Firmino amerudi katika hali yake ya kawaida kama ilivyo kwa Kevin Volland. Tutajilinda vizuri na tutapapa nafasi za kufunga”.
"Marcel Schmelzer na Erik Durm tunatarajia kuwa nao katika mechi hiyo.” Alihitimisha Klopp.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video