CARLO
Ancelotti amechizika baada ya Real Madrid kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Celta Vigo katika mchezo wa La Liga na kujitoa
rasmi katika mbio za ubingwa, huku wakisaliwa
na mchezo mmoja tu.
Endapo
wangeshinda, vijana hao wa Santiago Bernabeu wangepunguza pengo la pointi na kufikia
pointi mbili nyuma ya vinara Atletico na
pointi moja mbele ya Barcelona, lakini matokeo ya jumapili yanamaanisha
matumaini yamekwisha.
“Rasmi
tumekosa La Liga. Ni mashindano ya kwanza msimu huu ambayo hatuwezi kushinda na
itakuwa ni uongo kama tukajipa moyo,” Alisema Ancelotti baada ya mechi.
“Tulikosa
wachezaji wengi muhimu, kwahiyo haikua rahisi kujiandaa na mechi hii. Tumefungwa
mabao mawili mepesi kabisa, lakini tulijaribu kurudi mchezoni baada ya pale”.
“Tunatakiwa
kuangalia ya mbele, sasa tunajiandaa na
mchezo wa mwisho na fainali ya UEFA”.
Real
Madrid watakabiliana na Espanyo katika mchezo wa mwisho wa La Liga kabla ya
kuumana na Atletico Madrid katika mchezo wa fainali wa UEFA mei 24 mwaka huu
mjini Lisbon, Ureno.
0 comments:
Post a Comment