Mmeniangusha vijana: Kocha wa Atletico, Diego Simeone akilalamika wakati wa mechi.
UWEZO wa kuokoa michomo wa kipa wa Malaga, Willy Caballero usiku wa jana
umeinyima ushindi Atletico Madrid na kupunguzwa kasi katika mbio za
ubingwa wa la LIga baada ya safe ya kufungana boa 1-1 na timu hiyo
Uwanja wa Vicente Calderon.
Kipa huyo Muargentina alitunguliwa na Toby
Alderweireld aliyeunganisha kwa kichwa kona ya Jose Sosa, hilo likiwa
bao la kusawazisha baada ya Samuel kutangulia kuwafungia wageni dakika
ya 65.
Atletico iliyomkosa mfungaji wao bora, Diego Costa, ambaye ni majeruhi sasa ina kazi ya kupambana na Barcelona hadj mwisho kuwania taji.
Barcelona
inaendelea kushika nafasi ya pili kwa pointi zake 86 za mechi 37, nyuma
ya Atletico yenye pointi 89 za mechi 37 pia, wakati Real yenye 84 za mechi 37 ya tatu.
0 comments:
Post a Comment