MIAMBA
ya soka ya DR Congo, AS Vita wameanza vyema kampeni zao za ligi ya mabingwa
baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya miamba ya Misri, Zamalek,
mjini Kinshasa usiku wa jana.
Ni
wiki moja tu imepita tangu maafa yalipotokea katika uwanja huo, lakini AS Vita
waliweza kuwafumua Zamalek wenye uzoefu mkubwa wa michuano hiyo.
Tukio
hilo la mashabiki kupoteza maisha lilitokea katika mchezo wa ligi kuu ya
Congo, kati ya AS Vita dhidi ya
wapinzani wao wakubwa TP Mazembe ambapo wenyeji walilala bao 1-0.
Katika
mchezo wa jana, bao la kwanza la AS Vita lilifungwa na Ndombe Mubele dakika ya
19 kipindi cha kwanza na goli hilo lilidumu mpaka dakika za lala salama.
Moamen
Zakaria aliisawazishia Zamalek bao hilo dakika ya 80 na ubao wa magoli kusomeka
1-1 na kuwapa matumaini makubwa Mafarao hao.
Dakika
mbili tu baadaye, AS Vita waliandika bao la pili na la ushindi kupitia kwa
Emmanuel Ngudikana na kuwafanya wacongo hao wawe kileleni mwa kundi A.
Wiki
hii, Zamalek wataikaribisha Al Hilal ya Sudan , wakati TP Mazembe na Vita
watakutana katika DRC `Dabi`.
0 comments:
Post a Comment