Tuesday, April 15, 2014

Ryan Giggs 1
Na George Mlanzi..
Yapata miaka 23+ tangu aanze kukipiga katika kikosi cha kwanza cha Manchester United hivyo sishangai kusikia akiitwa the greatest ever player, inavyoonekana nikama huu ndo utakuwa mwezi wake wa mwisho pale Old Trafford. Baada ya kukipiga zaidi ya mala 962.
Ryan Giggs, akiwa ametia kibindoni umri upatao miaka 40, nasikia mkataba wake utafikia tamati mwishoni mwa msimu huu.
Lakini kabla hajaachana na jabulani ni busara kama nikimpa heshima yake hasa ukizingatia kawafunika wanaume kama akina Sir Bobby Charlton mwanaume ambae alifanikiwa kukipiga mala 758 akiwa na Manchester United hii ilikuwa record ya hatari lakini mwanaume Giggs aliivunja yapata miaka mitano iliyopita pale Moscow, wakati anashinda taji kubwa yani European Cup akiwa na United.
Kwa hesabu za faster faster Giggs amecheza mala 190 zaidi ya ma legends wote wakali wa United yani Eric Cantona, Cristiano Ronaldo pamoja na Nemanja Vidic.
Hakuna ubishi kuwa Cantona alikuwa more decisive pale Old Trafford, huku George Best alikuwa more talented wakati Denis Law wenye timu Yao wanamuita “King of the Stretford End,” lakini Giggs atakuwa na mengi ya kumuelezea mala tu atakapotundika njumu zake.
Pamoja nakuwa jamaa hakuwa striker, lakini Bado anashika nafasi ya Saba kwa wafumania nyavu bora waliopata kutokea akiwa ametoboa nyavu mala 168.
Kama haitoshi Giggs amekipigq mala 151 akiwa na club moja kwenye Champions League, zaidi ya mchezaji MWINGINE yeyote.
Mwanaume kakipiga zaidi kwenye club yake kuliko hata Paolo Maldini wa AC Milan.
Nilimshuhudia Giggs akianza dhidi ya Bayern Munich pale Old Trafford katika 16 bora kwenye Champions League, huku mchango wake mkubwa ukiwa dhidi ya Olympiakos, ambapo alicheza dakika 90 nakufanikiwa uisaidia United kupindua matokeo ya 2-0.
Anyway yapo mengi sana lakini nimechoka kuandika hebu nikumbushe yakwako ambayo unayakumbuka kwa huyu kiumbe.
Mimi nasepa zangu kujiandaa na semi final huku Ba akiwa kwenye form ya hatari

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video