Wednesday, April 2, 2014

PIX 1 (3)Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali WOINSO, Bi. Janeth Sebastian (katikati) akifafanua jambo juu ya kazi mbalimbali zifanywazo na Shirika lake wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msaidizi wake Bi. Namsifu Singo na kushoto ni Katibu wake Bi. Consolota Simon.
PICHA  NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO
…………………………………………………………………….
Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
 
SHIRIKA lisilo la Kiserikali Women in Society (WOINSO) linatarajia kuzindua mpango wa Elimu juu ya athari ya magonjwa ya ngono, utoaji mimba na mahusiano mashuleni kwa shule za msingi darasa la sita na la saba.
 
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Shirika hilo Bi. Janeth Sebastian wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa Habari Maelezo uliopo jijini Dar es Salaam.
 
Bi. Janeth amesema kuwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam Shirika lake linazindua mpango huo Kiwilaya na baadae wanatarajia kuzindua pia katika Wilaya ya Ilala na Temeke ikiwemo na mikoa mingine kama Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Songea.
 
Bi. Janeth ameongeza kuwa Elimu itakayotolewa juu ya athari ya magonjwa ya ngono, utoaji mimba na mahusiano mashuleni kwa shule za msingi darasa la sita na la saba na Daktari Mwelimishaji italenga kuwapa uelewa wanafunzi na kuwafanya wajitambue kwa yale watakayofundishwa na hivyo kuwaepusha vijana hao na athari mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza kwao.
 
“Elimu hiyo watakyopewa wanafunzi wa darasa la Sita na Saba itawawezesha kuwafanya wajitambue kwa yale watakayofundishwa na hivyo kuwaepusha vijana hao na athari kama vile magonjwa yatokanayo na ngono, utoaji mimba unaosababisha vifo na ugumba na mahusiano kabla ya wakati”. Alisema Bi. Janeth.
 
Aidha, Bi. Janeth amewasisitiza wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari kuhudhuria Uzinduzi rasmi utakaofanyika ukumbi wa Shekina Garden uliopo Mbezi Beach Makonde jijini Dar es Salaam siku ya tarehe 3/04/2014 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Meh. Yusuph Mwenda.
 
WOINSO ni Shirika lisilo la Kiserikali lililosajiliwa chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto kwa namba00NGO/00006564 mwaka 2013. Kabla ya usajili mkubwa lilikuwa linaelimisha kwa usajili maalumu na limefanya kazi tokea mwaka 2011 ambapo makao yake makuu yapo Dar es Salaam.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video