BONDIA
Wladimir Klitschko ameendeleza ubabe wake katika ndondi za uzito wa juu
baada ya usiku wa kuamkia leo kumchapa kwa Knockout (KO) ya raundi ya
tano, Alex Leapai katika pambano la kutetea mataji yake.
Klitschko,
alitumia mikono yake mirefu kumchapa kama 'mwanawe' mpinzani huyo wa
Samoa mzaliwa wa Australia, ambaye raundi ya tano alisalimu amri katika
pambano lililofanyika mjini Oberhausen, Ujerumani Magharibi.
Leapai alikwenda chini baada ya kuchanganyiwa makonde ya mikono yote, kushoto naa kulia mfululizo.
Aliinuka
kujaribu kutaka kuendelea, lakini kwa nia nzuri, Klitschko raia wa
Ukraine akajisogeza mbali zikiwa zimesalia sekunde 58 raundi hiyo
kumalizika.
Pokea
hiyo: Konde la Klitschko likichapa kidevu cha Leapai jana katika
pambano la ubingwa wa dunia uzito wa juu mjini Oberhausen, Ujerumani
Magharibi.
Chini: Klitschko akimuangalia mpinzani wake, Leapai anavyopambana na sakafu
Mataji
kibao: Wladimir Klitschko akisherehekea ushindi wake dhidi ya Alex
Leapai ambao umemfanya atetee mataji yake ya WBA, IBF, WBO na IBO
0 comments:
Post a Comment