ASERNE
Wenger amesema bado ataendelea kuwepo Asernal msimu ujao wa ligi kuu nchini
England na tayari ameshawaambia viongozi wake kuhusu jambo hilo.
Mfaransa
huyo hajasaini mkataba wa miaka miwili alioongezewa katika mkataba wake wa sasa
tangu oktoba mwaka jana.
Asernal
inasemekana kuwasiliana na Louis van Gaal kufuatia kutokuwa na uhakika wa kuwa
na Wenger siku za usoni, lakini Mholanzi huyo amewaambia marafiki zake kuwa yuko
makini kufuatilia dili la kumrithi David Moyes , Manchester United.
Hata
hivyo, Wenger alipokuwa akizungumza na beIN
Sport alithibitisha kuwa anataka kukaa London: “Nimezungumza mara nyingi,
nimeshaiambia klabu kuwa nataka kuendelea kuwepo hapa”.
Pia
Wenger amezungumzia maisha ya makocha katika mpira wa Kiingereza baada ya David
Moyes kufukuzwa na kusisitiza kuwa hawapewi muda kabisa.
“Kama
unataka watu bora sehemu yoyote, lazima uwape muda wa kujiboresha na kuwa bora
kama utakavyo” alisema Wenger.
“Watu
bora hawaji baadaye. Maisha ya makocha wa ligi kuu ni miezi 11. Muda mfupi sana”.
Aidha,
Bosi huyo wa Arsenal alisema alishangazwa sana na jinsi Manchester United
walivyolishugulikia jambo la Moyes ambapo alishuhudia magazeti mengi yakiripo
suala hilo kabla ya klabu kuthibitisha.
“Inashangaza
sana. Katika hali kama hii, inatakiwa kocha kuwa mtu wa kwanza kujua.
Unazungumza naye ana kwa ana, lakini inakuwa kama ugomvi”.
0 comments:
Post a Comment