Monday, April 14, 2014


Mgombea wa nafasi ya Ubunge kutoka mwaka wa pili, Bwana Okoka akimwaga sera zake kwa wapiga kura ambao ni wanafunzi wa shule ya Uandishi wa habari na mawasiliano kwa Umma SJMC iliyopo chini ya chuo kikuu cha Dar es salaam-UDSM. 
Kampeni za Uchaguzi wa serikali ya wanafunzi DARUSO-SJMC utakaofanyika jumatano (aprili 16) mwaka huu zimezinduliwa rasmi  leo  majira ya saa 7 mchana na mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi, Bwana Michael Christopher.
 Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi  na Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa serikali ya Wanafunzi DARUSO-SJMC, Bwana Michael Christopher aliratibu zoezi la uzinduzi wa kampeni ambaPo wagombea wote wa nafasi mbalimbali walipata fursa ya kumwaga sera zao.
 Naibu Waziri wa Mikopo wa serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Dar es salaam,  DARUSO anayemaliza muda wake, Bwana Damian Wambura maarufu kwa jina la Shishi.com alikuwepo wakati wa kampeni hizo ambapo alipata nafasi ya kuzungumza machache baada ya wagombea wa nafasi zote kumaliza kuwamga sera zao. Shishi alifafanua kuwa katika uongozi wake amejitahidi kuwasaidia wanafunzi waliokuwa na matatizo ya mikopo hususani kucheleweshewa fedha za kujikimu kutoka Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu.

 Wanafunzi walikuwa makini kusikiliza sera za wagombea ili kujua nani anawafaa na nani ni `chenga`
Mbunge mstaafu, Bwana Samuel Kamugisha, Mwanafunzi wa mwaka wa tatu (wa kwanza kulia) akifurahia jambo wakati wa kampeni hizo. Aliyeshika tama ni Trustgod Simbila, mwanafunzi wa mwaka wa pili akikunwa na sera za Bwana Okoka (hayupo pichani)
 Mwanafunzi wa mwaka wa tatu, Noelia J Gatera (mwenye `earphone`) akisikiliza na kuchambua sera za wagombea mbalimbali ili kujua nani wa kumpatia kura yake muhimu kwa mstakabali wa SJMC ya kesho.
 Atatikisa pochi yake: Mgombea wan nafasi ya Ukatibu mkuu Bwana Mmari Kennedy akieleza sera zake kwa wapiga kura (hawapo pichani) ambapo alisema katika uongozi wake ataanza kushughulikia suala la malazi kwa wanafunzi wa SJMC.
Pia amesema kama atapewa nafasi hiyo atakuwa na utaratibu wa kuwakutanisha wanafunzi wa SJMC kuanzia mwaka wa kwanza mpaka wa tatu na wataalumu waliopo katika fani zao, lengo likiwa ni kuwaongezea uzoefu zaidi na kujua hali ya mazingira ya kazi mtaani.
Aidha aliongeza kuwa atahakikisha michezo inaboreshwa chuoni hapo, huku akimwaga ahadi ya kugharamia maji kwa wachezaji wa timu za chuo kila zinapocheza kwa kutoa fedha za mfukoni mwake.
 Mwanafunzi wa mwaka wa pili ambaye pia ni mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi cha Michezo,  redio Mlimani ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, Francis Kivuyo akiuliza swali
 Wagombea wa nafasi mbalimbali wakiwa ndani ya chumba chao kabla ya kwenda kumwaga sera kwa wapiga kura. Hapa kila mtu alienda kivyake.
 Mwanadada huyo naye yupo katika ulingo wa uchaguzi. Hataki kuwezeshwa hata kidogo
 Wanafunzi wa mwaka wa tatu, Mahamud Rajab ( wa kwanza kushoto), Zainab Ngambila (wa pili kushoto), Ibrahim Masae `Ibra Cheche` (wa tatu kushoto) na Juma Dennis  (wa kwanza kulia), wakiwa na mambo yao wakati wagombea wakieleza sera zao. Hawa jamaa inaonekana wamechoshwa na siasa ukizingatia wana kazi kubwa ya kufanya tafiti za kubebea `Magamba` mwaka huu.
 Mbunge mstaafu, Bwana Samuel Kamugisha, Mwanafunzi wa mwaka wa tatu alikuwa kinara wa kuuliza maswali wa wagombea. Na hivi amewahi kuwa ndani ya DARUSO, hakika wagombea waliumiza vichwa mno kwa maswali yake kigongo.


PICHA NA MPENJA BLOG

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video