WACHEZAJI
wa Barcelona wametembelea eneo maalum lililoandaliwa na klabu kwa ajili ya
kutoa heshima za mwisho kwa aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Tito
Vilanova aliyefariki jana ijumaa.
Vilanova
aliyekuwa kocha msaidizi wa Pep Guardiola kabla ya kuwa kocha mkuu amefariki
akiwa na miaka 45 kutokana na maradhi ya saratani ya koo.
Baada
ya kurithi mikoba ya Guardiola msimu wa 2012/2013, Vilanova aliiongoza
Barcelona kutwaa ubingwa wa La Liga kwa pointi 100 na kuweka rekodi.
Hata
hivyo kazi yake nzuri iliingiliwa na maradhi na kulazimika kujiuzulu mwezi
julai mwaka jana.
Klabu
ilithibitsha jana kuwa Vilanova amefariki na leo hii wachezaji na makocha
wakiwa wageni wa kwanza, wametembelea eneo maalum liliotengwa kwa shughuli ya
kutoa heshima za mwisho kwa Tito.
Kocha
mkuu Gerardo Martino akiwa na mkurugenzi mkuu Andoni Zubizarreta na rais Joesp
Maria Bartomeu waliiongoza klabu kutoa salamu za rambirambi.
“Baada
ya kusaini kitabu cha rambirambi, kikosi kizima kilienda kuitazama picha kubwa
ya Tito Vilanova, ambapo walikaa kimya kwa muda kama sehemu ya kutoa heshima
kwake”. Barca wameandika kwenye Tovuti ya klabu.
“Ilikuwa
hali ngumu sana kwa wachezaji kumuona kocha wao aliyewafundisha wengi wao
katika soka la ujana na akiwa msaidizi wa Pep na baadaye kuwa kocha mkuu”.
Nahodha
Carles Puyol alisema: “Kutoka hapa tunatuma salamu za pole kwa familia na
marafiki”.
Milango
ya eneo hilo katika uwanja wa Camp Nou imeshafungulia kwa watu wote kwenda
kutoa heshima zao za mwisho kwa Tito.
0 comments:
Post a Comment