BEKI wa Chelsea, David Luiz amejifunga bao na kuwanufaisha zaidi Paris Saint-Germain katika ushindi wa nyumbani wa mabao 3-1 usiku huu katika mechi ya kwanza ya robo fainali, ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Lavezzi alianza kufunga karamu ya mabao kwa PSG katika dakika ya 4 ya kipindi cha kwanza. Dakika ya 27, Hazard aliisawazishia Chelsea bao hilo kwa njia ya mkwaju wa penati na kwenda mapumziko matokeo yakiwa 1-1.
Kipindi cha pili, nyota ya mabingwa wa Ufaransa iliendelea kung`ara ambapo dakika ya 62, David Luiz alijifunga na kuufanya ubao wa matokeo usomeke 2-1.
Wakati Chelsea wakihaha kutaka kusawazisha bao hilo, dakika ya 90 ya mchezo, Javier Pastore aliandika baoa la tatu na kuwanyamazisha ghafla mashabiki wa wazee wa darajani.
Baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, Kocha wa Chelsea alisalimiana isivyokuwa kawaida yake na benchi la ufundi la PSG, lakini haijajulikana kama amewakubali sana au vipi.
Zilisalia dakika 28 pekee kwa Chelsea kutoa sare, lakini bao la kujifunga la Luiz liliwachanganya na kubadili upepo wa mchezo. Na kabla ya hapo walikuwa wamejiamini kufanya vizuri.
Kikosi cha PSG: Sirigu 6, Jallet 6.5, Alex 6.5, Thiago Silva 6, Maxwell 6.5, Verratti 6 (Cabaye 76), Thiago Motta 6.5, Matuidi 6.5, Cavani 7, Ibrahimovic 6 (Lucas Moura 68), Lavezzi 8 (Pastore 84).
Kikosi cha Chelsea: Cech 5.5, Ivanovic 6, Cahill 6, Terry 6, Azpilicueta 6, Ramires 6, Luiz 6.5, Willian 6.5, Oscar 6 (Lampard 72), Hazard 7, Schurrle 5 (Torres 59).
Majanga: John Terry, David Luiz, Petr Cech na Cesar Azpilicueta wakiduwaa baada ya kujifunga bao la pili
Oh hapana! Luiz hakuweza kuuzuia mpira usizame nyavuni
Kufungwa kubaya, cheki Luiz anavyoshangaa baada ya kuwafungia PSG bao la pili usiku huu
Msumari wa mwisho: Javier Pastore akishangilia bao la tatu usiku huu
Faida kwa PSG: Pastore akizingirwa na wenzake baada ya kufunga bao la tatu
Hakuna furaha tena: Jose Mourinho akifoka
Kapelekwa sokoni: Hazard akimpoteza kipa wa PSG , Salvatore Sirigu na kuandika bao la kusawazisha kwa penati pekee waliyopata
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia bao lao
Katika mechi nyingine iliyochezwa usiku huu, Real Madrid waliwaalika Borussia Dortmund katika uwanja wa Santiago, Bernabeu na kushuhudia wajerumani hao wakipigwa mabao 3-0.
Mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo ameifikia rekodi ya mabao ya hasimu wake Lionel Messi wa Barcelona katika ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kufunga bao lake la 14 usiku huu , hivyo kuifikia rekodi hiyo ya mabao 14 ya Messi katika msimu mmoja wa UEFA.
Ronaldo ambaye hakuwa katika kiwango chake alifunga bao la tatu katika ushindi wa leo, lakini alitoka uwanjani baada ya kupata majeruhi na kuwafanya mashabiki wote wa Real Madrid kusimama na kumpigia makofi wakati anakwenda benchi.
Katika mechi yake ya 100 ya ligi ya mabingwa, Ronaldo amefikisha mabao 49 aliyowahi kufunga Alfredo Di Stefano katika michuano ya Ulaya.
Pia Ronaldo katika mchezo wa leo alimsaidi Gareth Bale kufunga bao la kwanza.
Kikosi cha Real Madrid: Casillas, Carvajal, Pepe, Sergio Ramos, Fabio Coentrao, Modric, Alonso, Isco (Illarramendi 71), Bale, Benzema (Morata 75), Ronaldo (Casemiro 80).
Mabao yamefungwa na: Bale 3, Isco 27, Ronaldo 57.
Kikosi cha Borussia Dortmund: Weidenfeller, Piszczek (Schieber 67), Hummels, Papastathopoulos, Durm, Kehl (Jojic 74), Sahin, Grosskreutz, Mkhitaryan (Hofmann 64), Reus, Aubameyang.
Kazi nzuri: Gareth Bale akifunga bao la kuongoza kwa Real Madrid
Jembe: Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefunga bao lake la 14 katika msimu mmoja wa UEFA
Anaunguruma: Cristiano Ronaldo akishangilia bao lake
CHANZO: SPORTSMAIL
0 comments:
Post a Comment