Kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba imetangaza kuwa mchakato wa
uchaguzi
wa klabu hiyo utaweza kuendelea baada ya msajili wa vyama vya
michezo
kuipitisha rasimu ya katiba ya Simba iliyopelekwa hivi
karibuni.
Mwenyekiti
wa kamati hiyo Damas Ndumbaro amesema kamati yake ilikaa
Alhamisi
wiki hii na kujadili masuala mbalimbali kuhusiana na mchakato
wa
uchaguzi ambao awali ulipangwa kufanyika mapema mwezi ujao.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Simba Damas
Ndumbaro amewataka
wanachama
wa klabu ya Simba kuvuta subira hadi hapo msajili wa vyama
vya
michezo atakaposaini rasimu ya katiba ndipo watakapo tangaza
kuanza
rasmi kwa harakati za kuwania nafasi mbalimbali ndani ya klabu
hiyo.
Ndumbaro
pia ambaye ni mwanasheria kitaaluma ametoa ufafanuzi kuhusu
madai
ya baadhi ya wanachama kutaka kutumia katiba ya zamani katika
uchaguzi
mkuu ujao.
0 comments:
Post a Comment