BAO
la dakika za mwishoni la Lima limeipa ushindi mwembamba Benfica katika
Nusu Fainali ya kwanza ya Europa League dhidi ya Juventus usiku wa
kuamkia leo.
Benfica
sasa itakuwa na mtihani wa kuulinda ushindi huo katika mchezo wa
marudiano dhidi ya vigogo hao wa Serie A wiki ijayo mjini Turin. Juve
inawania taji la kwanza la Ulaya baada ya miaka 17.
Lima
alipokea pasi ndani ya boksi na kuwafungia wenyeji bao la ushindi
dakika ya 84, baada ya Carlos Tevez kutoka kuisawazishia Juve dakika ya
72 katika mchezo ambao beki wa kati Ezequiel Garay alitangulia kuifungia Benfica bao la kuongoza dakika ya pili.
Katika
mchezo mwingine wa Nusu Fainali ya michuano hiyo, Sevilla imeifunga
Valencia 2-0, mabao ya Mbia dakika ya 33 na Bacca dakika ya 66.Bao muhimu; Carlos Tevez akishangilia baada ya kuifungia bao la ugenini Juventus ikilala 2-1 Benfica |
0 comments:
Post a Comment