CHELSEA
wana imani kuwa beki wao mkongwe, John Terry atakubali kusaini mkata mwingine
utaomfanya awepo mpaka msimu ujao, amesema kocha msaidizi Steve Holland ijumaa
hii.
Beki
huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya England ameripotiwa kupewa ofa ya mkataba
mpya, lakini mshahara wake utakuwa nusu ya mshahara apatao sasa.
Hata
hivyo, Holland amegoma kuzungumzia makubaliano na beki wao huyo mwenye miaka
33, wakati huo huo akieleza kuwa wakongwe wengine, Frank Lampard na Ashley Cole
wapo mbioni kusaini mikataba mipya.
“John
amekuwa na msimu mzuri; ameifanya beki yetu iwe katika kiwango bora na yeye
amekuwa akifanya kazi hiyo”.
“Najua
John anataka kubaki Chelsea na Chelsea inamhitaji John, kwahiyo nadhani
makubaliano yatafikiwa wiki chache zijazo”.
“Kama
ilivyo kwa John, naye Lampand na Cole watapewa heshima hiyo. Hawa ni wachezaji
wa muda mrefu hapa klabuni na nadhani tunawapa heshi makubwa”. Alisema Holland
katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mechi ya kesho dhidi ya
Sunderland.
Chelsea
kwasasa wapo katika nafasi ya pili kwenye msimamo, pointi mbili nyuma ya Liverpool wenye
pointi 77 kileleni.
0 comments:
Post a Comment