SIR ALEX FERGUSON atashiriki kikamilifu katika mchakato wa
kumpata Meneja mpya wa Manchester United kuziba nafasi ya David Moyes
aliefukuzwa.
Moyes, ambae alipendekezwa na Sir Alex Ferguson ili kumrithi
baada ya yeye kustaafu, alifukuzwa kazi Jumanne baada ya kudumu Miezi 10
tu.
Safari hii, Ferguson atakuwa mmoja wa Watu kadhaa, hasa
Wakurugenzi wa Bodi ya Man United, watakaoshiriki mchakato mzima wa
kumpata Meneja mpya badala ya yeye pekee kupendekeza Jina kama
alivyofanya alipoteuliwa Moyes.
Hivi sasa Man United inaongozwa na Meneja wa Muda, Ryan Giggs,
ambae ni Kocha-Mchezaji wa Klabu hiyo na anasaidiwa na Wachezaji wenzake
wa zamani Nicky Butt, aliekuwa akifundisha Timu ya Rizevu na Phil
Neville, aliekuwa Msaidizi chini ya Moyes lakini hii Leo imetajwa kwamba
Paul Scholes nae amejumuika kwenye Jopo hilo la Benchi la Ufundi.
Pia, Man United imesema inaendelea kuchambua yupi atafaa kuwa
Meneja wao wa kudumu huku Vyombo vya Habari huko England vikigusia kuwa
wenye nafasi kubwa ni Kocha wa Netherlands, Louis van Gaal na Meneja wa
sasa wa Real Madrid, Carlo Ancelotti.
Home
»
»Unlabelled
» SIR ALEX KUSHIRIKI KUSAKA MRITHI WA MOYES MAN UNITED
Thursday, April 24, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment