Wednesday, April 23, 2014

394238_heroa
KOCHA wa Atletico Madrid, Diego Simeone ameieleza suluhu ya leo dhidi ya Chelsea kuwa imewapa unafuu mkubwa wapinzani wake kuelekea katika mchezo wa marudiano nchini England.
Vinara hao wa La Liga walicheza mpira mzuri, lakini walishindwa kupenya ngoma ya ulinzi ya Chelsea licha ya krosi nyingi kupigwa katika eneo la hatari la the Blues.
Diego Costa alishindwa kufanya maarifa ya kufunga kipindi cha kwanza, wakati mpira wa adhabu uliopigwa na nahodha Gabi uliokolewa vizuri na kipa aliyeingia kuchukua nafasi ya Cech, Mark Schwarzer.
Beki na nahodha wa Chelsea, John Terry alitoka kipindi cha pili baada ya kupata majeruhi ya enka, lakini Simeone anaamini wapinzani wake watakuwa na furaha zaidi kwao Stamford Bridge wiki ijayo.
“Ulikuwa mchezo mgumu na kila mtu alishindwa kupata matokeo” Alisema Margenina huyo.
“Tulishindwa kupata bao la ushindi. Ilikuwa mechi ngumu kwa timu zote kwasababu zinapambana kufika fainali”.
“Wana faida na suluhu hii, lakini yeyote atakayeshinda mechi ijayo ataenda fainali”.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video