KLABU ya Villarreal imempiga marufuku ya kudumu ya
kutoingia katika uwanja wake wa El Madrigal shabiki aliyemrushia ndizi beki wa
kulia wa FC Barcelona, Dani Alves kwenye mchezo wa La Liga jana jumapili.
Beki huyo wa kibrazil baada ya kurushiwa ndizi
hiyo aliiokota na kuila wakati akiwa katika harakati za kupiga kona, na kitendo
hicho kilionesha shukurani za kejeli kwa shabiki aliyefanya jambo hilo la
kibaguzi.
Katika mechi hiyo Barca walitoka nyuma kwa mabao
2-0 na kushinda 3-2.
Villarreal wamethibitisha kumpa kifungo cha kidumu
shabiki huyo na kusitisha tiketi zake za msimu huu, huku wakitarajia
kumchukulia hatua kali zaidi juu ya ishara ya ubaguzi wa rangi aliyoionesha
jana.
“Villarreal inaitangazia dunia kuwa imekerwa sana
na kuchukizwa na kitendo kilichotokea jana kwenye mechi dhidi ya FC Barcelona
ambapo shabiki alirusha ndizi katika uwanja El Madrigal”. Taarifa ya klabu
imesomeka.
“Shukurani kwa maafisa usalama na mashabiki wote.
Klabu imefanikiwa kumbaini shabiki huyo na kuamua kufuta tiketi zake za msimu
huu na kumfungia kifungo cha kudumu kutoingia katika uwanja wa El Madrigal”
“Kwa mara nyingine tena, klabu inapenda kueleza
msimamo wake juu ya heshima, usawa, undugu na mchezo wa kiungwana ndani na nje
ya uwanja na haitavumilia uvunjifu wa kanuni hizi kama vile kuleta fujo na ubaguzi
wa rangi”.
Kitendo alichofanyiwa Alves jana kimemkera Mbrazil
mwenzake aliyeweka picha katika mitandao ya kijamii akila ndizi kama ishara ya
kumuunga mkono kaka yake huyo mweye miaka 30 na kuandika maneno chini ya picha
yaliyosema: “Sisi wote ni nyani”.
Mabao mawili ya kujifunga na lile la Lionel Messi
yaliwafanya Barca kwa mbali waanze kufufua matumaini ya kutwaa ubingwa katika
wiki hii ngumu ambayo wamempoteza kocha wao wa zamani, Tito Vilanova.
0 comments:
Post a Comment