Mfalme; Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kufunga usiku huu, Real Madrid ikiichapa 4-0 Osasuna
MABAO
mawili ya Cristiano Ronaldo katika ushindi wa 4-0 wa Real Madrid dhidi
ya Osasuna usiku wa jana, yamemfanya atimize mabao 30 na kuongeza matumaini
ya timu yake kutwaa ubingwa.
Cristiano
Ronaldo alifunga bao la kwanza dakika ya sita kwa pasi ya Angel di
Maria kabla ya kuongeza la pili dakika ya 52 kwa pasi ya Isco na Sergio
Ramos akafunga la tatu dakika ya 60 kwa pasi ya di Maria kabla ya Daniel
Carvajal kufunga la nne dakika ya 83 pasi ya Isco.
Ushindi
huo, unaifanya Real itimize pointi 82 baada ya kucheza mechi 34 na
inaendelea kukamata nafasi ya pili nyuma ya vinara Atletico Madrid wenye
pointi 85 za mechi 34, wakati Barcelona yenye pointi 81 za mechi 34 pia
ni ya tatu.
0 comments:
Post a Comment