Mambo shwari: Karim Benzema akishangilia bao pekee aliloifungia Real Madrid katika ushindi wa bao 1-0.
Benzema (kushoto) akifunga bao huku beki wa Bayern David Alaba
Kipa wa Real Madrid , Iker Casillas akiokoa mchomo dakika za mwisho kumnyima bao la kusawazisha Mario Gotze
Kazi ngumu: Pep Guardiola (kulia) akionekana kukosa furaha baada ya kupoteza mechi Bernabeu
BAO pekee la Karim Benzema katika dakika ya 19` limeipatia ushindi muhimu Real Madrid katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe hilo, klabu ya Bayern Munich kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid nchini Hispania.
Bao hilo limewapa nguvu Real Madrid na kuwaongezea morali kueleka katika mchezo wa marudiano jumanne ya wiki ijayo katika dimba la Allianz Arena.
Kama Real Madirid watachuku kombe mwaka huu basi watakuwa wamechukua taji hilo mara 10.
Kocha Carlo Ancelotti na timu yake wangepata mabao mengi katika mechi ya leo na kuwa na uhakika wa kufika fainali ya UEFA tangu waliposhinda taji hilo mwaka 2002.
Cristiano Ronaldo na Angel di Maria walikosa nafasi nzuri za kufunga na sasa wamejipa kazi ngumu Allianz Arena kwasababu Bayern Munich ni timu hatari na haitataka kuvuliwa ubingwa kirahisi kwao.
Kikosi cha Real Madrid: Casillas, Carvajal, Fabio Coentrao, Alonso, Pepe (Varane 73), Ramos, Modric, Isco (Illarramendi 82), Benzema, Di Maria, Ronaldo (Bale 74)
Kikosi cha Bayern Munich: Neuer, Rafinha (Javi Martinez 66), Alaba, Kroos, Boateng, Dante, Robben, Lahm, Mandzukic, Schweinsteiger (Muller 74), Ribery (Gotze 72)
Mechi hiyo imechezeshwa na mwamuzi Howard Webb kutoka nchini England.
0 comments:
Post a Comment