-
Iker CasillasAlifanya kazi nzuri ya kumnyima bao la kusawazisha mshambuliaji wa Bayern, Mario Gotze katika dakika za mwisho. Alilinda kwa ustadi lango lake na kutofungwa.
-
PepeBeki huyo raia wa Ureno alicheza vizuri na alikuwepo kila eneo kuisaidia timu yake. Kwa ujumla amecheza kwa ubora.
Sergio Ramos
Alisaidiana vizuri na Pepe, alijilinda kukwepa kadi ya njano, lakini alionesha upinzani na kuokoa hatari chache.
-
Fabio CoentraoAlicheza vizuri kipindi chote cha mchezo, alipambana na Robben na kupiga krosi chache.
-
Daniel CarvajalAlimzuia vizuri Alaba ili asipande kupiga krosi , pia alimbana vizuri Ribbery na kushindwa kuisaidia klabu yake kupata matokeo.
-
Alikuwa katika kiwango chake na kuonesha uzoefu wake sehemu ya kiungo . Alimyima raha kabisa Muller kufanya vitu vyake. Alitibua vizuri mipira ya hatari katika eneo lake
-
Luka ModricAlimiliki mpira vizuri na kuwa mtu muhimu katika dakika za mwisho ambapo Real walikuwa wanazuia wasifungwe bao. Alionesha kiwango kizuri kwa muda wote wa mchezo
-
Alishindwa kupiga krosi na kukimbia na mipira kutoka sehemu ya kiungo na alikosa nafasi kipindi cha kwanza. Licha ya haya, alionesha kiwango kizuri.
-
IscoAlionesha uwezo wake, alisumbuana na Robben na kusababisha faulo nyingi, laini alifanya kazi yake vizuri
-
C. RonaldoHukupiga mashuti sana golini na alimjaribu vizuri Neuer mara moja. Haukuwa usiku mzuri kwake kwani hakuwa katika kiwango chake, lakini kama kawaida alimpa pasi nzuri Coentrao iliyozaa bao.
-
Karim Benzema Top of the MatchAlifunga bao zuri na kucheza vizuri.
-
Aliokoa michomo kadhaa na kuhakikisha Real Madrid hawafungi magoli mengi na kuwapa taabu mechi ya marudiano
-
DanteMbrazil alicheza vizuri lakini alishindwa kuzuia mpira wa krosi uliosababisha bao
-
RafinhaAlicheza vizuri nafasi ya beki wa pembeni na kupiga krosi mara kadhaa na alikabiliana vizuri na Coentrao aliyekuwa anapanda kupiga krosi.
-
Jerome BoatengAlihusika katika matukio mengi na kujikuta akicheza chini ya kiwango katika michuano hii mikubwa barani Ulaya
-
Philipp LahmAlimiliki mpira vizuri na ilikuwa bahati mbaya kwake kwasababu angefunga bao kipindi cha kwanza baada ya kukimbia vizuri na mpira.
-
David AlabaAlitulia na mpira na kupiga basi murua. Pia alimsaidia vizuri Ribery kila inapowezekana.
-
Franck RibéryMpira ulimkataa mfaransa huyu, hakupiga shuti lolote na alishindwa kabisa kumchomoka Carvajal . Ilikuwa sahihi kutolewa kipindi cha pili.
-
Arjen RobbenMtu hatari zaidi wa Bayern, lakini hakupata nafasi ya kufunga. Alicheza vizuri akitokea kulia na kujaribu mara nyingi, lakini mabeki wa Real Madrid walikuwa imara
-
Bastian SchweinsteigerHakuwa na mchango mkubwa leo hii, lakini alimiliki vizuri mpira. Alijaribu kupiga mipira miwili miepesi ya adhabu ndogo
-
Toni KroosAlijaribu mashuti mawili yaliyozuiliwa na mabeki, lakini bado alionesha ubora wake wa kupiga basi
-
Mario MandzukicAlijaribu kupambana na mipira mingi ya kichwa, lakini Pepe na Sergio Ramos walimbana vizuri. Alishindwa kumjaribu Casillas.Viwango hizi havijahusisha wachezaji walioingia kutokea benchi
0 comments:
Post a Comment