Pigo: Madrid inaweza kumkosa Bale na Cristiano Ronaldo leo
WINGA
Gareth Bale yuko shakani kuichezaea Real Madrid katika Nusu Fainali ya
Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya mabingwa wa Ujerumani, Bayern
Munich kutokana na kusumbuliwa nugonjwa wa mafua.
Nyota huyo wa Wales hajasafiri na wenzake kwa ajili ya mchezo wa kwanza leo Uwanja wa Sangtiago Bernabeu.
Kocha
wa Real Madrid, Carlo Ancelotti pia anatilia shaka uzima wa Cristano
Ronaldo. Nyota huyo wa Ureno anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya muda
mfupi kabla ya mchezo wa leo.
Ikiwa
Bale ataukosa mchezo wa leo, litakuwa pigo kwa Ancelotti, ambaye
alimwagia sifa nyingi winga huyo katika Mkutano na Waandishi wa Habari
kuelekea mchezo wa leo.
Bale
anang'ara kwa sasa, baada ya kufunga bao la ushindi katika fainali ya
Copa del Rey dhidi ya Barcelona wiki iliyopita na kocha wake akasema
mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 86 kutoka Tottenham
atakuwsa mkali zaidi msimu ujao Hispania ambao utakuwa wa pili kwake
Real.
"Gareth
ni mtoto mkali,"alisema Ancelotti. "Anavutia kwa kujiamini kiasi cha
kutosha hususan kutokana na bao alilofunga dhidi ya Barcelona katika
fainali,"alisema.
0 comments:
Post a Comment