Mwenyekiti wa chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) Jamal Emil Malinzi amewasili leo Alhamis tarehe 10-4-2014 saa nne asubuhi katika Uwanja wa ndege wa Bukoba Mjini na kupokelewa na Wadau wengi, Huku ikiwa ni mara ya kwanza tangu achaguliwe Rais wa TFF.
Bw. Jamal Malinzi baada ya kutua amezungumza na Viongozi wa Soka Mkoani hapa Kagera na baadae kuhudhulia Kikao cha kamati Tendaji ya KRFA na siku inayofuata utakuwepo mkutano mkuu wa KRFA.
Bw. Jamal Malinzi baada ya kutua amezungumza na Viongozi wa Soka Mkoani hapa Kagera na baadae kuhudhulia Kikao cha kamati Tendaji ya KRFA na siku inayofuata utakuwepo mkutano mkuu wa KRFA.
Kulia ni Bw. Pelegrinius .A. Rutayuga, Mjumbe wa kamati Tendaji ya KRFA , Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF na Mshauri Mkuu wa Kiufundi TFF makao makuu, nae alikuwepo Uwanja wa Ndege Bukoba kwa mapokezi ya Rais wa TFF Ndugu Jamal Malinzi. Na hapa wakiteta jambo kwa kushirikishana na wadau pamoja na Viongozi.
Rais wa shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Ndugu Jamal Malinzi
Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Emil Malinzi kwenye picha na Mwandishi wa Mtandao wa Jamii Bukobasports.com leo muda mchache alipotua kwenye Uwanja wa Ndege mjini Bukoba leo.

0 comments:
Post a Comment