Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana usiku ametunuku nishani na Tuzo kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa na watumishi wa umma wapatao 86 waliotoa mchango wao katika kuulinda na kuudumisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliodumu kwa miaka Hamsini 50.Mama Maria Nyerere akipokea nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano(Order) kwa niaba ya Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Mama Maria Nyerere Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungnao Daraja nne.
Mama Fatma Karume akipokea Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano(Order) kwa niaba ya Marehemu Abeid Aman Karume Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Mama Fatma Karume nishani ya kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja Nne wakati wa hafla ya kutunuku nishani na tuzo za miaka 50 Muungano zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Mh.Benjamin William Mkapa Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano(Order) wakati wa sherehe ya kutunuku nishani na tuzo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.(picha na Freddy Maro)
0 comments:
Post a Comment