Monday, April 14, 2014


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

0712461976 

BAADA ya kitendawili cha ubingwa kuteguliwa jana ambapo Azam fc wamewapiga bao Yanga na kutwaa mwari wa ligi kuu soka Tanzania bara, mechi moja tu yenye mvuto imebaki kufunga pazia la ligi kuu msimu huu wa 2013/2014.
Mechi hii si nyingine bali ni baina ya timu za Prisons dhidi ya Ashanti United ambazo zitapambana aprili 19 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kutafuta timu moja itakayoungana na Rhino Rangers na JKT Oljoro kushuka daraja.
Utamu wa mechi hii unakuja katika mazingira ya aina mbili;
Mosi; timu zote zimecheza mechi 25 na kujikusanyia pointi 25. Kinachozitofautisha ni mabao ya kufunga na kufungwa.
Prisons wamecheza mechi 25 ambapo wameshinda mechi 5, sare 10 na kupoteza mechi 10.
Wajelajela hao wamefumania nyavu mara 25 na kufungwa mabao 33. Ukitoa mabao ya kufunga na kufungwa unapata hasi (-8).
Ashanti United wameshinda mechi 6, sare 7 na kufungwa mechi 12.
Wamefunga mabao 20 na kufungwa mabao 38. Ukitoa mabao ya kufunga na kufungwa anapata hasi kumi na nane (-18).
Kwa wastani huo wa mabao ya kufunga na kufungwa, Prisons wanakuwa juu ya Ashanti United.
Katika msimamo, Prisons wapo nafasi ya 11, huku nafasi ya 12 ikikaliwa na Ashanti United, lakini zimefungana pointi.
Kuelekea katika mechi hiyo, klabu zote zinahitaji ushindi, lakini Ashanti ndio wahitaji wakubwa zaidi kwasababu wamezidiwa mabao mengi ya kufunga na Prisons.
Endapo Ashanti United watashinda mechi hiyo watafikisha pointi 28 na kuvuka mkasi wa kushuka daraja, wakati Prisons watakuwa wameshashuka daraja.
Matokeo ya sare ya aina yoyote ile yatawashusha daraja Ashanti kwasababu ya wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Kwahiyo matokeo pekee ya maana kwa kocha wa Ashanti, Abdallah Kibadeni ni kushinda, vinginevyo itakuwa imekula kwake.
Kama Prisons watapata sare siku hiyo, watakuwa wamenusurika kushika daraja kwa faida ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Kwa mazingira haya, mechi hii itakuwa na soka la ushindani kupiata maelezo ikizingatiwa timu zote zimetoka kushinda mechi zao za mwishoni wa wiki iliyopita.



Jumamosi Prisons walishinda mabao 4-3 dhidi ya Rhino Rangers kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, wakati jana Ashanti walishinda bao 1-0 dhidi ya Simba sc katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Pili; utamu wa mechi hii unatokana na kupigwa uwanja huru;.
Prisons na Ashanti United zinatumia viwanja tofauti kwa mechi za nyumbani.
Ashanti wanatumia dimba la Azam Complex jijini Dar es salaam, wakati Prisons wanatumia Sokoine jijini Mbeya City.
Kwa mazingira hayo, timu zote zitakuwa ugenini ambapo mashabiki wao watalazimika kusafiri na kwenda kuzishangilia timu zao.
Kutoka Mbeya kwenda Morogoro kunahitaji maandalizi kwa shabiki, ili hali kutoka Dar kwenda Morogoro.
Kwa mazingira haya mashabiki yawezekana wasiwe wengi kama ambavyo ingetokea kwa Chamazi au Sokoine nne.
Wataoenda kushangilia timu hizi watakuwa ardhi ya ugenini, hivyo italeta ladha nzuri ya mchezo huo.
Tatu; ubora wa makocha wa timu hizo mbili na jinsi walivyozisadia timu kufika hapo zilipo.
Yawezekana Ashanti wangekuwa wameshashuka kama Rhino kama si kuingia kwa Kibadeni.
`King` amefanya kazi kubwa kuinusuru klabu hiyo iliyokuwa katika hali tete mzunguko wa kwanza na mwanzoni mwa mzunguko wa pili.
Ujio wa Kibadeni umeleta ahueni kwa Ashanti mpaka sasa inapambana mpaka dakika ya mwisho.
Kocha kibadeni alishasema kuwa hana cha kupoteza zaidi ya kushinda mechi mbili za mwisho kuanzia ya jana dhidi ya Simba sc ambayo alipata matokeo mazuri.
Sasa amebakiwa na mechi moja na Prisons, na inawezekana mikakati yake ni mkubwa mno kuhakikisha anashinda.
Naye kocha mkuu wa Prisons, David Mwamwaja aliikuta timu ikiwa hoi chini ya kocha Jumanne Chale ambaye ameishusha  daraja Rhino Rangers.
Lengo la Prisons kumfukuza Chale ilikuwa kutafuta kocha atayeinuru kushuka daraja na ndipo walifanya uchaguzi sahihi wa kumpa mikoba Mwamwaja.
Chini ya Mwamwaja, Prisons imefanya vizuri na kufikia hapo ilipo.
Malengo ya Mwamwaja hayajatimia kama kwa Kibadeni, kwani wote walipewa timu ili wazinusuru kushuka daraja.
Sasa hali imefikia patamu ambapo makocha wenye malengo yanayofanana wanakutana katika mechi moja.
Kila mtu atahitaji kushinda na kufunga mabao mengi, hivyo mechi itakuwa nzuri mno.
Mtandao huu utaendelea kukujuza kila kinachoendelea kuelekea mechi hii atakayoamua timu gani iungane na Rhino na JKT Oljoro kushuka daraja msimu huu.
Stand United ya Shinyanga, Ndanda fc ya Mtwara na Polisi Morogoro zinasubiri timu tatu zishuke ili msimu ujao zijivinjari katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara baada ya safari ngumu ya ligi daraja la kwanza.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video