Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
BAADA
ya kurejea ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015, klabu ya
Polisi Morogoro ameanza tambo za kuja na muonekanao mpya.
Afisa
habari wa klabu hiyo, Clemence Banzo ameueleza mtandao huu kuwa wapo
katika mikakati mikubwa ya kuijenga timu yao kwa kusajili wachezaji
chipukizi na kuimarisha masuala ya utawala mithiri ya Mbeya City FC.
“Kiukweli Mbeya City wametupa fundisho kubwa sana. Mafanikio yao yametugusa, na ipo haja ya kuiga nyayo zao”.
“Kwanza
tunatarajia kufanya usajili usiojali majina kama wao. Pili tunaanza
maandalizi ya mapema ili kujiimarisha zaidi”. Alisema Banzo.
Banzo
aliongeza kuwa Polisi Moro ya sasa itakuwa tofauti na ya zamani
kwasababu wanataka kuipeleka zaidi kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro.
‘Mashabiki
ni nguzo muhimu sana katika soka, angalia Mbeya City jinsi walivyo na
nguvu kwasababu ya watu wengi kuwa nyuma yao. Nasisi Polisi tunaona ipo
haja ya kuipeleka timu hii kwa wananchi”.
“Tunaanza
mchakato wa kufungua matawi maeneo tofauti nchini, lengo likiwa ni kuwa
na uhusiano wa karibu na mashabiki wetu”. Alisema Banzo.
Aidha,
afisa habari huyo alisema kuwa wamefanya kazi kubwa kurudi ligi kuu,
hivyo wanataka kufanya jitihada za kushiriki kwa muda mrefu.
“Ni
rahisi kushuka daraja, lakini kurudi ni changamoto kubwa. Tunamshukuru
Mungu ndani ya mwaka mmoja tumerudi ligi kuu, lakini changamoto iliyopo
mbele yetu ni kuwa na timu ya ushindani na si ushiriki”. Alisema Banzo.
Polisi Morogoro ni moja ya timu tatu zilizopanda kushiriki michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015.
Timu nyingine ni Ndanda fc ya Mkoani Mtwara na Stand United ya shinyanga.
Timu zilizoshuka daraja ni Rhino Rangers ya Tabora, JKT Oljoro ya Arusha na Ashanti United ya Dar es salaam.
Ujio wa Ndanda fc unatabiriwa kuwa mzuri kutokana na uzalendo wanaounesha mashabiki wa soka mkoani Mtwara.
Baada
ya timu hiyo kupanda ligi kuu, mamia ya mashabiki walijitokeza kuipokea
timu uwanja wa ndege na kupanga foleni barabarani kuishangilia
inapopita mitaani.
Baada
ya hapo walianzisha slogani ya `Ndanda fc kwa roho safi`, inayomaanisha
wanaisapoti timu yao kwanza na kuachana na Simba na Yanga.
Hata
watu wa Shinyanga wameonekana kuwa na furaha kubwa na timu yao kupata
nafasi ya kucheza ligi kuu, hivyo wanatarajiwa kuiunga mkono kama ilivyo
kwa wakazi wa Mbeya.
Kama timu hizi zitapata nguvu kama ya Mbeya City fc basi itakuwa changamoto nyingine kwa timu za juu, Azam fc, Yanga na Simba.
0 comments:
Post a Comment