Na Saidy Mdoe, Dar es Salaam
MWANAMUZIKI mkongwe mwenye historia ya kipekee katika muziki wa Tanzania, Muhidin Maalim Gurumo amefariki dunia leo saa 9 mchana.
Habari kutoka ndani ya familia ya Mzee Gurumo zimeiambia Saluti5 kuwa mwimbaji huyo amefariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kwamba jana usiku Gurumo aliugua ghafla na kukimbizwa Muhimbili kabla mauti kumkuta leo mchana. Taarifa hizo zinasema Gurumo alikuwa akilalamika moyo kumuuma.

Pumzika kwa amani; Mzee Muhiddi nGurumo enzi za uhai wake |
Gurumo alizaliwa mwaka 1940 na historia yake kimuziki ikaanzia mwaka 1960 kupitia bendi Kilimanjaro Chacha kabla ya kujiunga Rufiji Jazz Band mwaka 1962.
Mwaka 1963 akajiunga na Kilwa Jazz Band kabla ya mwaka 1964 kuwa mmoja wa waasisi Nuta Jazz “Msondo Ngoma” (baadae ikawa Juwata Jazz) akaitumikia hadi mwaka 1978 alipokwenda tena kuanzisha DDC Mlimani Park “Sikinde” .
Mwaka 1985 akajiunga na Orchestra Safari Sound (OSS) na kuasisi mtindo wa Ndekule ngoma ya Mababu. Akadumu kwa miaka mitano kabla ya kurejea tena Msondo mwaka 1990 alipodumu hadi mwaka jana alipotangaza kustaafu muziki.
Wiki iliyopita uvumi wa kufa kwa Gurumo lakini Saluti5 ilipompigia simu mwimbaji huyo alipokea simu na kuongea katika hali iliyoonyesha yuko fiti.
Saluti5 itakujulisha taratibu za mazishi zitakavyokuwa. Jambo moja ambalo Gurumo aliwahi kuliweka wazi kwa Saluti5 ni kuwa akifariki lazima akazikwe kijijni kwao Masaki – Kisarawe.
CHANZO:TOVUTI YA SALUTI 5.
0 comments:
Post a Comment