
MANUEL
Pellegrini ameanza harakati za kumuwinda beki wa kati wa Sampdoria
inayoshiri ligi kuu nchini Italia, Seria A, Shkodran Mustafi.
Beki
huyo mahiri alitemwa na kocha wa Manchester United mwaka 2012 wakati
huo akiwa na Everton kwa madai ya kutokuwepo katika mipango yake.
Bosi huyo wa Manchester alisema mchezaji huyo kijana hakukidhi vigezo vyake Goodison Park na kumruhusu kuhama bure.
Mustafi kipindi akiwa na Moyes katika klabu ya Everton alicheza mechi moja tu, nayo alianzia benchi.
Pia beki huyo anapirotiwa kuwindwa na Juventus, baada ya kuwa na msimu mzuri Sampdoria na kucheza mechi 31 katika mashindano yote msimu huu.
Mustafi alipewa nafasi mara moja ya kuchezea timu ya Taifa ya Ujerumani baada ya kocha Joachim Low kumwita mwezi februari mwaka huu wakati Ujerumani ilipocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Chile.
Manchester
City wanataka kuimarisha safu yao ya ulinzi baada ya Matija Nastasic
kusumbuliwa zaidi na majeuhi, wakati huo huo Joleon Lescott akitarajia
kuondoka bure majira ya kiangazi mwaka huu kufuatia mkataba wake
kumalizika na klabu kutokuwa na mpango naye.
0 comments:
Post a Comment