Wednesday, April 30, 2014


 Katika kipindi cha masaa 24 mabingwa wa Tanzania bara klabu ya Azam FC imeipa mapigo mawili takatifu wapinzani wao Dar Young Africans baada ya kufanikiwa kumsajili mshambuliaji Didier Kavumbagu jana na leo hii Azam wamekamilisha rasmi usajili wa kiungo Frank Domayo.

Domayo amesaini mkataba huo akiwa jijini Mbeya na timu ya Taifa ya Taznzania, Taifa stars inayojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi itakayochezwa mei 4 mwaka huu uwanja wa sokoine jijini Mbeya.

Hizi ni harakati za Azam fc kujiimarisha kueleke michuano ya kimataifa mwakani na kutetea ubingwa wao.

Taarifa rasmi zilizotolewa na klabu ya Azam ni kwamba Domayo amesaini mkataba wa miaka miwili wa kujiunga na mabingwa wa VPL baada ya kumaliza mkataba wake

Katibu mkuu wa Azam, Nassor Idrisa `Father` amekaririwa akisema wapo katika utekelezaji wa ripoti ya kocha wao Joseph Marius Omog ambaye aliwataka kuimarisha maeneo kadhaa ya kikosi.

Omog alisema wasajili kiungo wa ulinzi, beki na mshambuliaji.

Kavumbagu ndani ya nyumba, Domayo naye kanasa, nani anafuata?

 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video