Kocha wa FC Barcelona , Gerardo Martino amemtetea
Lionel Messi kufuatia watu wengi kuzisi kumkosoa mchezaji huyo bora wa dunia
mara nne baada ya kuonesha kiwango kibovu katika mchezo wa marudiano wa robo fainali
ligi ya mabingwa barani Ulaya jamatano ya wiki hii dhidi ya Atletico Madrid.
Katika mchezo huo, Barca walifungwa bao 1-0 na
kutupwa nje ya mashindano kwa wastani wa mabao 2-1 kufuatia sare ya bao 1-1
kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Camp Nou.
“Ni ngumu sana kuwa kama Leo Messi katika maisha haya ya soka,”
amesema kocha Martino ambaye anatoka mji wa Messi wa Rosario nchini Argentina.
“Kimsingia hakuna kwake. Anapocheza kinyume na matarajio ya
wingi basi anakosolewa mno, lakini nadhani ni ngumu sana kuwa kama yeye”.
Aliongeza Martino wakati akizungumza na waandishi wa habari kueleka mchezo wa
kesho wa La Liga dhidi ya Granada.
0 comments:
Post a Comment