ZIKIWA
zimebaki saa chache kushuhudia timu itakayoungana na Real Madrid katika mchezo
wa fainali ya UEFA mei 24 mjini Lisbon nchini Ureno kati ya Chelsea au
Atletico, Jose Mourinho ametetea mbinu yake ya kupaki basi inayolalamikiwa na
makocha wengi.
Mourinho
amesema kuwa kuna falsafa nyingi za soka na anashangaa wanaolalamika juu ya
mbinu zake kwasababu asingefanya hivyo angekuwa anafungwa mara nyingi.
Kocha
huyo raia wa Ureno alilalamikiwa `kupaki basi` na Atletico Madrid kwenye uwanja
wa Vicente Calderon na kulazimisha suluhu ya bila kufungana.
Jumapili
iliyopita, alitumia mbinu kama hiyo na kuwafunga Liverpool mabao 2-0 uwanja wa
Anfield na kufufua matumaini kidogo ya kutwaa ubingwa, lakini kocha wa majogoo
wa jiji Brendan Rodgers alimlalamikia Mourinho kwa kupaki basi na kusema
anacheza mpira wa kizamani.
Japokuwa
wengi wanalalamika kuwa Chelsea wanatumia mbinu za zamani nje ya mpira wa
kisasa, Mreno huyo amewashangaa na kusema kikosi chake kina nguvu na kucheza
mpira safi.
Mourinho
katika mkutano na waandishi wa habari amesema: “Unajua, siku hizi kuna wataalumu
wengi wa soka na wanafahamu zaidi mpira kuliko mimi, wana mitazamo ya juu,
hakika inastaajabisha”.
“Lakini
ukweli utabaki kuwa ukweli: kama timu haijilinda vizuri na kufunga mabao mengi,
basi kutakuwa na tatizo kubwa”.
“Timu
bila usawa sio timu. Mpinzani anapokuwa na mpira lazima ujitahidi kumzuia
asikufunge. Tunapokuwa na mpira tunajaribu kufunga. Huo ndio mpira-mpira
ninaoujua”.
“Nakumbuka
nilisema mara ya kwanza nilipofika hapa, kama una kipa kama Petr Cech anayeweza
kupiga mpira mpaka kwenye boksi la mpinzani , halafu kuna mshambuliaji kama
Didier Drogba anayejaribu kila mpira wa juu, kwanini ucheze mipira mifupi? Ukifanya hivyo labda ni mpumbavu”.
“Kama
wapinzani wako wanashambulia sana kwa kushitukiza na kuna nafasi katika safu
yako ya ulinzi na unawapa nafasi utakuwa mpumbavu”
0 comments:
Post a Comment