ERICK MAGANA |
MCHEZO wa ngumi utachezwa Chalinze mkoa wa Pwani katika ukumbi wa Ndelema Inn ukiwakutanisha mabondia Erick Magana kutoka Dar es salaam atakaye oneshana umwamba wa kutupiana makonde na Mwaite Juma siku ya April 15 katika ukumbi wa Ndelema Inn Chalinze Mjini
mpambano huo wenye upinzani mkubwa wa ali ya juu unaosubiliwa na wapenzi wa ngumi Chalinze Mkoa wa pwani pamoja na vitongoji vya jirani utakuwa chachu ya kuhamasisha mchezo uho kwa ajili ya kuibua vipaji vipya vya mchezo wa ngumi katika mkoa mzima wa pwani
mbali ya mpambano huo kutakuwa na mipambano mingine ya utangulizi ambayo watapata wapinzani wao baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano huo utakaowakutanisha mabondia wa chalinze na Dar es salaam
mabondia ambao watatoka Dar kwenda kupambana na wenzao wa chalinze ni Erick Magana,Godfrey Sadiki ’Pacho Mawe’,Juma Biglee,Husein Pendeza,Hamisi Kavirondo, ambao wata ongozana na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’
kwa ajili ya kwenda kushiriki mashindano hayo ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi nchini mchezo ambao unapendwa na wengi duniani
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul ‘canelo’ alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila ‘Super D’ kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha
JUMA BIGLEE |
0 comments:
Post a Comment