MCHEZAJI kinda wa klabu ya Chelsea na raia wa
Tanzania, Adam Nditi ameilaumu serikali ya Tanzania kuwanyima haki watanzania
wengi walio nje ya nchi kuja kuitumikia nchi
katika fani mbalimbali kutokana na kushindwa kuruhusu uraia wa nchi mbili.
Katika mahojiano maalum, Nditi amesikitishwa na
serikali kushindwa kutoa uraia wa nchi mbili kwasababu wanaona uchungu kuona
nchi yao inafanya vibaya wakati wanao uwezo wa kutoa mchango wao.
“Binafsi kama serikali ya nchi yetu itaruhusu
uraia wa nchini mbili, niko tayari kuja kuichezea taifa stars hata kesho”.
Amesema Nditi.
Nditi ameendelea kufafanua kuwa wapo watanzania
wengi wenye fani mbalimbali kama vile wanasoka, madakatari na nyinginezo,
lakini wanashindwa kuja kuitumikia nchi kwasababu taifa halijakubali uraia wa
nchi mbili.
“kinachowasumbua watu wengi ni maslahi wanayoyapa
huku Ulaya”.
“Inakuwa ngumu kwa watanzania waliopo huku kuacha
kazi zinazowalipa vizuri na kuja nchini”.
“Lakini kama suala la uraia wa nchi mbili
litaruhusiwa, wengi watakuja”. Ameongeza Nditi.
Aidha, kinda huyo mwenye kipaji cha juu katika
klabu ya Chelsea amesisitiza kuwa ifike wakati serikali iwafirie na kuukubali
mfumo wa uraia wa nchi mbili kwani ni wajibu wa msingi kulisaidia taifa katika
fani tofauti.
“Nchi yetu ina upungufu wa madaktari na
wanamichezo bora, lakini wanashindwa
kuja kusaidia Taifa”.
“Nasisitiza serikali ituruhusu na sisi tuje
kuiokoa nchi yetu”. Amesema Nditi.
Nditi alizaliwa Zanzibar mwaka 1994 kabla ya
kujiunga na timu ya Chelsea ya chini ya miaka 13 miaka kadhaa iliyopita baada
ya kuhamia England na familia yake.
0 comments:
Post a Comment