KLABU
ya Napoli imekumbwa na wasiwasi mkubwa baada ya kuumia kwa Gonzalo Higuain
katika mechi yao na Inter Milan hapo jana uwanja wa San Siro iliyomalizika kwa
suluhu (0-0).
Mshambuliaji
huyo raia wa Argentina alilazimika kutoka katika mchezo huo wa Seria A baada ya
kugongana na beki wa Inter, marco Andreolli.
Napoli
wamethibitisha leo hii kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid amepata
majeruhi ya kifundo cha mguu na kuwa hatarini kukosa mechi ya Coppa Italia wiki
ijayo.
“Amepata
majeruhi makubwa sana kwenye mguu wake” amesema taarifa ya klabu.
“Majibu
hayo yametokana na uchunguzi uliofanywa na madaktari wa klabu juu ya hali ya
Gonzalo Higuain baada ya kugongana na Andreolli kwenye mechi ya Inter dhidi ya
Napoli”.
“Higuain
hayuko katika hali nzuri na tathmini zaidi ya afya yake itatolewa siku zijazo”.
Kocha
wa timu ya taifa ya Argentina, Alejandro
Sabella amesitushwa na majeruhi ya
Higuain na anaomba apone haraka kwasababu ni moja ya washambuliaji
atakaowatumia kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Mshambuliaji
huyo mwenye miaka 26 mpaka sasa amefunga mabao 24 katika mechi 44 alizocheza
tangu ajiunge na Napoli mwezi wa nane mwaka jana kwa uhamisho wa paundi milioni
40 kutoka Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment