WASHINDI
wa tatu msimu wa 2013/2014 wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya
Mbeya City ya jijini Mbeya kesho jumamosi inatarajia kufunga pazia la
ligi hiyo dhidi ya Maafande wa Mgambo JKT.
Hii
itakuwa mechi muhimu kwa kocha mkuu wa klabu hiyo Juma Mwambusi
kutokana na matokeo aliyoyapata wiki iliyopita dhidi ya Azam fc ambapo
alifungwa mabao 2-1 nyumbani na kuwapa ubingwa rasmi.
Endapo Mwambusi atashinda mechi ya kesho, basi itakuwa faraja kubwa kwake na kwa mashabiki wa klabu hiyo iliyoleta ushindani mkubwa mno msimu huu.
Mbeya
City FC mpaka sasa wamecheza mechi 25 na kujikusanyia pointi 46 katika
nafasi ya tatu ambayo tayari wamefanikiwa kuichukua.
Kwa
upande wa Mgambo JKT, wanauchukulia mchezi huo kwa uzito wa hali ya juu
ili kuweza kupata pointi tatu muhimu na kufikisha pointi 29.
Japokuwa
maafande hawa wapo nafasi ya 10 baada ya kucheza mechi 25 na
kujikusanyia pointi 26 na kujiweka mazingira mazuri ya kubaki ligi kuu,
lakini bado wanahitaji ushindi katika mechi ya kesho.
Kuelekea
katika mchezo huo, kocha mkuu wa msaidizi wa Mgambo JKT, Moka Shaban
Dihimba alisema kuwa wataingia kwa nia ya kupambana na kuibuka na
ushindi dhidi ya Mbeya City wenye machungu ya kufungwa.
“Tunajua wapinzani wetu ni wazuri sana hasa wanapokuwa nyumbani kwao”.
“
Kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Azam fc kunawafanya waje na nguvu
zaidi ya kutaka kushinda, lakini mpira una matokeo matatu, kufunga,
kufungwa na kutoa sare”
“ Tumejipanga kushinda, lakini tutakubaliana na matokoe yoyote”. Alisema Moka.
Naye Maka Mwalyiswi, Kocha msaidizi wa Mbeya City fc alisema nia ya siku zote ni kushinda.
“Malengo
ya Mbeya City fc katika mechi yoyote ni kushinda. Kila mechi tunaipa
uzito wa hali ya juu. Tulijiandaa kwa nguvu sawa katika michezo 26 ya
ligi kuu”.
“Kikosi chetu kipo katika hali nzuri na tunatarajia kucheza mpira mzuri na kushinda. Mashabiki wetu watuamini”. Alisema Maka.
Wakati
hayo yakijiri, afisa habari wa Mbeya City fc, Freddy Jackson amesema
kocha mkuu wa klabu hiyo, Juma Mwambusi amekerwa mno na anaendelea
kuhuzunishwa na tuhuma za yeye kuhongwa na Azam fc ili afungwe mechi iliyopita.
Jackson
amesema Mwambusi bado anaendelea kusikia watu wakimsema vibaya na
kumhukumu kwa kipigo cha 2-1 ambapo wanadai amehongwa nyumba chamazi.
“Kocha
wetu ni mtu mzima na amefundisha timu nyingi kwa mafanikio. Hongo ya
nyumba ni kubwa mno. Mwalimu anaumia sana kusikia maneno hayo”. Alisema
Jackson.
Jackson aliwaasa watu wanaendelea kumchafua Mwambusi kuachana na tabia hiyo kwasababu waliokuwepo uwanjani wanajua kilichotokoe.
“Timu
ilicheza mpira mzuri na ilikuwa na uwezo wa kushinda. Maamuzi mabovu ya
refa ndio yalitugharimu. Kwa soka lile, inakuingiaje akilini kuwa timu
ilihongwa? Tuachane na maneno yasiyokuwa na maana”. Aliongeza Jackson.
Kabla
ya kukutana na Azam fc Mbeya City ilituhumiwa kuppokea hongo kutoka wa
wana Lambalamba hao ili wacheze chini ya kiwango na kuwazawadia ubingwa.
Tuhuma
hizo zilikuwa ni klabu kuahidiwa kununuliwa basi, kocha Mwambusi
kujengewa nyumba chamazi na wachezaji kupewa fedha ili wacheze chini ya
kiwango.
Lakini Uongozi wa Mbeya City fc ulikanusha shutuma hizo na kuwataka mashabiki wao kuzipuuza kabisa.
0 comments:
Post a Comment