Na Mwandishi Wetu
MWENDESHA
baiskeli mahiri hapa nchini, Said Kengele ametoka na baiskeli kutoka
Tunduma jijini Mbeya hadi Dar es Salaam kwa baiskeli kwa lengo la
kusherehekea Sikukuu ya Muungano inayotarajia kuadhimishwa Aprili 26.
Kwa
mujibu wa Kengele safari kutoka Tunduma ilianza Aprili 10 akiwa
safarini amekumbana na changamoto ya uchakavu wa mipira ya baiskeli na
matairi.
Kengele
alisema changamoto nyingine ni milima na miteremko mikali akiwa
safarini ambako anatarajia kuwasili jijini Dar es Salaam Jumamosi ya
Aprili 19.
Aidha
Kengele ametokea Tunduma na baiskeli alipokwenda kwa ajili ya kutoa
hamasa katika mchezo huo kabla ya kuanza safari ya kurejea jijini Dar es
Salaam.
0 comments:
Post a Comment
Links to this post
Create a Link