Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MABINGWA
wa zamani wa Tanzania kwa mwaka 1999 na 2000, Mtibwa Sugar wamekiri
kukumbana na changamoto kubwa msimu wa 2013/2014 wa ligi kuu Tanzania
bara uliomalizika aprili 19 mwaka huu .
Afisha
habari wa klabu hiyo, Tobias Kifaru Lugalambwike ameueleza mtandao huu
kuwa kitu kikubwa walichojifunza ni maandalizi makubwa ya baaadhi ya
timu zinazoshiriki ligi kuu toafuti na wao.
“Sisi
ni wakongwe katika ligi hii, lakini tumeshindwa kuonesha cheche
kutokana na kuwepo kwa timu zenye kiwango kizuri. Mbeya City fc
wametikisa kweli, sio kwetu tu hata Simba na Yanga wamekumbana na
upinzani na ndio maana wamekosa ubingwa ”.
“Kikubwa
tumebaini changamoto zetu ikiwemo kukosa wachezaji muhimu kikosini.
Tunataka kufanya usajili mzuri ili tuanze maandalizi ya mapema”.
“Kufikia mwezi juni lazima mchakato wa mazoezi utaanza. Tumechoshwa na kuboronga isivyo kawaida yetu”. Alisema Kifaru.
Kifaru
aliongeza kuwa katika usajili wanaotarajia kufanya, kama kawaida yao
hawataangalia majina makubwa kwasababu Mtibwa ni kitalu cha kuzalisha
wachezaji.
“Tumekuwa
tukizalisha wachezaji bora wanaowaniwa na Simba na Yanga, lakini
hatuchoki kwasababu sisi ni kitalu. Tunahaha kutafuta nyota wengine
watakaotusaidia msimu ujao”. Alisema Kifaru.
Akizungumzia
maamuzi ya waamuzi msimu huu, Kifaru alisema kwa upande wao hawana
tatizo nao, lakini aliwataka kuboresha zaidi viwango vyao kwasababu kuna
wakati walikuwa wanaharibu uhondo wa mechi.
“Waamuzi
wamefanya kazi yao vizuri, tunajua yapo makosa ya kibinadamu. Cha
msingi wazichukue changamoto zao ili wazifanyie kazi kabla ya msimu
mpya kuanza”.
“Tunatarajia
ligi ngumu zaidi msimu ujao. Kuna timu za wananchi zimeshapanda ligi
kuu. Nadhani zinaweza kuwa kama Mbeya City, hivyo waamuzi lazima
wajisahihishe makosa yao mapema na kujipanga upya”. Alisema Kifaru.
Mtibwa Sugar msimu huu imemaliza katika nafasi ya 7 baada ya kujikusanyia pointi 31 kibindoni.
0 comments:
Post a Comment