Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akitoa hotuba yake wakati wa kukabidhi madawati 107 katika Shule ya Sekondari Pugu kupitia mpango alioluanzisha wa `Mayors Ball` ya kusaidia sekta ya elimu. Katikati ni Diwani wa Kata ya Pugu, Imelda Samjela, na kulia kwake ni Diwani wa Kata ya Upanga Magharibi, Jokha Lemki.
Katika hafla hiyo iliyofanyika shuleni hapo leo jijini Dar es salaam jana, madawati 300 yenye thamani ya sh. Milioni 45 yaligawiwa katika shule za Pugu, Ulongoni, Jangwani.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Pugu wakishuhudia makabidhiano ya msaada huo ambao kwa kiasi kikubwa utasaidia kutatua kero ya samani katika shule yao Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akipeana mkono na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Pugu, baada ya kuwakabidhi madawati 107 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Manispaa ya Ilala pamoja na Madiwani mara baada ya kukabidhi madawati hayo.Diwani wa Kata ya Pugu, Imelda Samjela akielezea changamoto mbalimbali zinazoikabili Shule hiyo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Huduma za Jamii Manispaa ya Ilala Angelina Malembeka, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu, Jovinus Mutabuzi na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa.
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
0 comments:
Post a Comment