Tuesday, April 29, 2014

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
CHAMA cha soka mkoani Mbeya, MREFA, kimeendelea kujivunia mafanikio ya kuaminiwa na shirikisho la soka Tanzania TFF kwa kuziweka timu za Taifa mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa MREFA, Elias Mwanjala ameuambia mtandao huu kuwa kuwekwa kambi ya maboresho ya Taifa stars mjini Tukuyu ilikuwa fursa nzuri kwa wafanyabiashara na wapenzi wa soka mkoani humo kuiona timu yao.
Mwanjala aliushukuru uongozi wa TFF chini ya rais Jamal Malinzi kwa kuendelea kuwapa fursa muhimu kama hizo na hasa baada ya kuamua mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Taifa Stars na Malawi kufanyika mkoni humo.
“TFF wanajua juhudi zetu. Uwanja wa Sokoine ulikuwa mbaya sana, lakini tumeuboresha kwa nguvu zote na sasa mechi ya kirafiki ya Taifa stars inafanyika katika uwanja huu. Hii ni heshima kubwa kwa MREFA”.
“Kwasasa tunajenga vyumba vya kubadilishia nguo vyenye hadhi ya kimataifa. Dhamira yetu ni kuwa na uwanja bora zaidi weye hadhi kubwa”. Alisema Mwanjala.
Taifa stars chini ya Kocha mpya, Mart Nooij aliongeza wachezaji tisa katika kikosi kilichochapwa mabao 3-0 na Burundi siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibara, aprili 26 mwaka huu uwanja wa Taifa.
Wachezaji hao waliongezwa kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi (The Flames) itakayochezwa Mei 4 mwaka huu katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. 
Wachezaji walioongezwa ni Edward Charles Manyama (JKT Ruvu), Elias Maguli (Ruvu Shooting), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Javu (Yanga), John Bocco (Azam), Kelvin Friday (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa).
Kwasasa Stars ipo kambini mjini Tukuyu na siku mbili kabla ya mechi hiyo itarudi mjini Mbeya tayari kwa maandalizi ya mwisho.
Akizungumzia timu za Prisons na Mbeya City fc, Mwanjala alisema zimejitahidi kupambana msimu uliopita wa ligi kuu ingawa zimeishia maeneo tofauti.
“Mbeya City tulianza kupotea baada ya kufungwa na Yanga, Coastal na mwisho Azam fc”.
“Timu haikuwa na uzoefu, lakini msimu ujao tutakuwa mabingwa kwasababu tutakuwa wazoefu”.
“Kwa Prisons kidogo uzoefu mdogo walionao umewabakisha ligi kuu, kikubwa ni kuziandaa timu hizi ili msimu ujao zifike mbali”.
“Prisons ilipoteza kete zake mzunguko wa kwanza, lakini raundi ya pili ilicheza soka zuri sema bahati haikuwa yao.” Alisema Mwanjala.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa wanajitahidi kuisaidia timu nyingine ya Kimondo fc ili iingie ligi kuu.
 “Tuna imani Kimondo fc itaweza kupanda ligi kuu, lakini kumbuka tuna timu nyingie ya Wenda fc, mabingwa wa mikoa”
“Wanaenda kushiriki ligi ya mabingwa wa mikoa, tunaamini itafuzu kucheza  ligi daraja la kwanza”. Aliongeza Mwanjala.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video