Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MRISHO Mpoto `Mjomba` amewaonya vijana wanaopenda njia za mkato katika kusaka mafanikio.
Mpoto
ameueleza mtandao huu kuwa mafanikio yana njia zake, hivyo lazima
vijana wakubali kujituma zaidi katika kazi zao ili kutimiza ndoto zao na
si kufikiria kufanikiwa kwa muda mfupi.
“Mjomba
njia za mkato ni hatari. Vijana hasa wanasanii wenzangu wasipende njia
za mkato. Lazima wafanye kazi na kuwa na subira ili wakati wao ufike”.
Alisema Mpoto.
Mjomba
aliongeza kuwa vitendo vya wasanii vijana kujihusisha na biashara ya
dawa za kulevya na matendo mengine ya uovu wanaufanya muziki uonekane wa
wahuni tu.
“Kijana unawekwa dawa tumboni sijui kwenda China na kwingineko. Mimi nadhani ni kuwa na haraka ya maisha”.
“ Tuacheni njia za mkato, twendeni njia ndefu tutafika tu japokuwa tutaona kama tunachelewa”. Alisema Mpoto.
Akiwazungumzia
watu maarufu wakiwemo wanasiasa na wafanya biashara wakubwa kuwatumia
vijana katika biashara haramu ya dawa za kulevya Mpoto alisema:
“Hawa
jamaa Mjomba hawafai kabisa, Sijui tuwape jina gani. Nikisema ni
wanyama, naona halina uzito. Ngoja niwatafutie jina lao mjomba”.
Aidha, Mpoto alisema wasanii wanatakiwa kujenga utaratibu wa kusoma vitabu ili wawe na ufahamu wa kutunga mashairi.
“Wasanii wengi Mjomba hawasomi. Wanakosa taarifa na ndio maana kila mtu anaimba mapenzi”.
“
Hivi kweli Mjomba kuna suala la mapenzi tu? Hapana! Yapo mengi ya
kuimba, lakini vijana hawana taarifa mjomba”. Alisema Mpoto.
Pia aliawaasa vijana kuwa na utamaduni wa kupenda vitu vyao na kuachana na kuiga mambo ya kigeni.
“Nasema mjomba tena na tena, utandawazi umetufanya tuwe watumwa.”.
“Angalia vijana wetu wanavyovaa mjomba! Ni aibu kubwa”.
“Mjomba hivi kweli usanii lazima uvae vimini, milegezo?, hapana mjomba, turudi katika tamaduni zetu”
“ Sisemi wasivae nguo za kisasa, lakini nadhani wanatakiwa kukumbuka maadili yetu”
Akizungumzia wimbo wake wa `Waite`, Mjomba alisema ameamua kuuweka katika hali nzuri kifani na maudhui.
“Watu wengi walikuwa wananilaumu, ooh! Mjomba nyimbo zako unajikita zaidi kwenye maudhui zaidi ya fani”.
“Sasa nikaona ni vyema kuja kivingine. Ukisikia mdundo wa Waite, hakika mjomba naupenda sana”.
“Lakini
nilivyoona mdundo ni wa nguvu, nami nikaingia ,..nikaingia Mjomba
..nikasema Waite wakalishe mjomba..hahahahahah”. Alisema Mpoto na
kucheka.
Ni msanii wa muziki wa dansi, filamu, mwongozaji, ngonjela, mshairi, na sanaa ya ngoma kutoka hapa nchini.
Mjomba ameimba nyimbo mbalimbali kama vile Salam Zangu Mjomba, Nikipata Nauli aliyoimba na Banana Zorro na sasa anatamba na kibao cha Waite.
Mjomba ni mmoja kati ya waanzilishi wa kundi la muziki la Parapanda.
0 comments:
Post a Comment