
MASHETANI
wekundu, Manchester United wamekuwa na msimu mbaya mwaka huu tangu
David Moyes aingie Old Traffod kurithi mikoba ya Sir Alex Ferguson na
sasa anaendelea kuvunja rekodi mbalimbali klabuni hapo.
Baada
ya kufungwa mechi ya jana mabao 2-0 na Everton uwanja wa Goodison Park,
Man United hawawezi kumaliza ligi katika nafasi ya nne na kwa maana
hiyo watakosa michuano ya UEFA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1995.
Ushindi wa jana uliwafanya Everton kwa mara ya kwanza kushinda nje ndani dhidi ya Man United tangu mwaka 1969-70.
Hapo
chini ni orodha ya rekodi zilizovunjwa na Moyes ambazo zilichapishwa na
mtandao wa Goal.com baada ya Man United kulala mabao 3-0 dhidi ya
Manchester City mwishoni mwa mwezi machi mwaka huu, lakini Moyes amendelea kuvunja rekodi zingine msimu huu
MOYES’S UNWANTED RECORDS AT MAN UTD
|
![]() |
United kwa mara kwanza wanamaliza ligi wakiwa nafasi ya chini tangu ligi kuu England kuanzishwa.
|
![]() |
United wanashindwa kufuzu michuano ya UEFA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1995
|
![]() |
United wamefanya vibaya zaidi nyumbani baada ya miongo kadhaa kupita
|
![]() |
Wamefungwa mara tatu mfululizo msimu huu tangu 2001.
|
![]() |
Wametolewa raundi ya tatu katika kombe ka FA Cup kitu kilichotokea mara moja wakati wa Ferguson
|
![]() |
Kufungwa kwa mara ya kwanza na Swansea City wakiwa Old Trafford.
|
![]() |
Kufungwa kwa mara ya kwanza nyumbani na Newcastle tangu mwaka 1972
|
![]() |
Kufungwa kwa mara ya kwanza nyumbani na West Brom tangu 1978
|
![]() |
Mechi ya kwanza ya ligi kupoteza dhidi ya Stoke tangu mwaka 1984
|
![]() |
Mara ya kwanza kwa Man United kufungwa bao la mapema zaidi ligi kuu –bao la Dzeko walipokabiliana na Manchester City
|
![]() |
Mara ya kwanza kwa Man City na Liverpool kumpiga nje ndani Man United Tangu Premier League kuanza
|
![]() |
|
![]() |
Mara ya kwanza Everton kumfunga Man United nje ndani tangu mwaka 969-70
|
0 comments:
Post a Comment