DAVID Moyes amewashukuru mashabiki wa Manchester United baada ya kufukuzwa kazi jana na kusema anajivunia kuiongozo klabu kubwa duniani kama Man United.
Moyes
alifukuzwa kazi kufuatia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Everton na
kuisababisha klabu hiyo ishindwe rasmi kufuzu michuano ya UEFA mwakani
na kumaliza ligi ikiwa katika nafasi ya chini zaidi tangu ilipofanya
hivyo msimu wa 1989-90.
Kupitia
kwa chama cha makocha wa ligi kuu nchini England, Moyes amesema:
“Kuteuliwa kuwa kocha wa Manchester United, moja ya klabu kubwa duniani,
bado itabaki kuwa kitu maalumu kwangu na nitajivunia daima”.
“Kubeba
mikoba ya klabu iliyokuwa katika mafanikio makubwa kwa muda mrefu
nilijua itakuwa changamoto kubwa kwangu, lakini kamwe sikuogopa kuchukua
kibarua hicho”.
“Kazi ya ukocha United ni ngumu, lakini daima mimi na wasaidizi wangu tulifanya kazi kwa bidii. Nawashukuru kwa kutumia muda mwingi katika kazi na kuwa waaminifu kwa klabu”
“Tulikuwa na malengo na tulijitoa kuijenga klabu, japokuwa katika kipindi hiki cha mpito, matokeo ya timu yalikuwa ni mabaya kwa mashabiki wa Man United tofauti na walivyotarajia”
0 comments:
Post a Comment