KOCHA Mkuu wa Mashetani wekundu, Manchester United, David Moyes amemuambia mwamuzi wa Hispania, Carlos Carballo kutoa maamuzi sahihi katika mchezo wao dhidi ya mabingwa wa Ulaya na Bundesliga, Bayern Munich kutokana na tabia ya wachezaji wa timu hiyo kujiangusha.
Man United inakabilina na Bayern usiku wa leo uwanja wa Old Trafford katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali, Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Bayern inapewa nafasi kubwa ya kushinda, lakini timu hiyo ya kocha Pep Guardiola ilishutumiwa baada ya kuitoa Arsenal katika raundi iliyopita, huku kocha wa washika bunduki wa London, Arsene Wenger akimlaumu Arjen Robben kuwa ni hodari wa kujirusha kujiangusha.
Moyes alisema: “Tunawaamini marefa watafanya uamuzi sahihi. Kujirusha ni moja ya vitu vibaya vya kufanyia kazi. Ningependa kutahadharisha juu ya hilo, lakini nisingependa kumlenga mchezaji binafsi,”.
Winga Mholanzi Anayepaa: Nyota wa Bayern, Arjen Robben amekuwa akishutumiwa kwa kujiangusha kirahisi
Angalizo la tahadhari: Kocha wa Manchester United, David Moyes anatumai refa Carlos Velasco Carballo atwaadhibu wachezaji wa kujiangusha
United imekuwa ikiumizwa na maamuzi ya marefa siku za karibuni katika michuano ya Ulaya, na winga Nani alitolewa kwa kadi nyekundu dhidi ya Real Madrid mwaka jana wakati beki Rafael alitolewa pia dhidi ya Bayern mwaka 2010.
Wajerumani hao tayari wamekwishatetea ubingwa wa Bundesliga na wameshinda mechi zao 27 kati ya 30 zilizopita kwenye mashindano yote. Lakini Ryan Giggs bado anaamini United inaweza kufika fainali.
Muongo mkubwa: Arsene Wenger alimshutumu Robben kwa tukio hili alipojiangusha wakati alipokutana na kipa Wojciech Szczesny katika raundi iliyopita
0 comments:
Post a Comment