JOSE
Mourinho amegoma kuzungumzia kuhusu kikosi atakachopanga katika mchezo wa ligi
kuu soka nchini England baina ya klabu ya Chelsea dhidi ya Liverpool jumapili
ya wiki hii katika dimba la Anfield.
Siku
za karibuni, Mreno huyo alikaririwa akisema atapanga kikosi dhaifu katika mechi
hiyo ili kuwapumzisha wachezaji wake nyota kuelea nusu fainali ya pili ya ligi
ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Atlectico Madrid jumatano ya wiki ijayo uwanja wa Stamford Bridge.
Mourinho
alipoulizwa kuwa anaidharau ligi ya England mpaka apange kikosi dhaifu?, kocha
huyo, 51, alisema mambo ya timu yake aachiwe yeye.
“Siku
zote kuchagua kikosi kitakachocheza ni siri ya kocha, Kama mtu anauliza swali
hilo, siwezi kumjibu”.
“Kitu
cha msingi ni klabu yangu na mashabiki wetu. Nahita
ji
kuilinda klabu na mashabiki wa Chelsea”.
“Kama
hatusaidiwi kutimiza ndoto zetu na malengo yetu, basi kuna sababu ya kutuacha
tufanye mambo yetu. Subirini jumapili na mtajua timu itakayocheza” Alisema
Mourinho.
Kocha
huyo wa zamani wa Real Madrid alipoulizwa kama mashabiki wa Chelsea
watafurahishwa na mabadiliko ya kikosi, alijibu kuwa mashabiki wa Stamford
Bridge watakuwa na imani na maamuzi.
Mourinho
alieleza kuwa leo hii hakuwa huru katika mkutano na waandishi wa habari
kufuatia adhabu aliyopewa na chama cha soka cha England, FA baada ya kumpongeza
mwamuzi Mike Dean aliechezesha mechi ya Chelsea dhidi ya Sunderland na
kushuhudia paka weusi wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0.
FA
wameyachukuliwa maneno ya Mourinho kama kejeli, lakini yeye anachukuliwa
kivingine.
Aliongeza:
“Kila ninapozungumza kuna madhara, hata kama nikisema mwamuzi amefanya kazi
nzuri napewa adhabu, kwahiyo sina uhuru kabisa. Kama mnataka mkutano mzuri
nendeni mkazungumze na FA na sio mimi”.
Pia
Mourinho amethibitsiha kuwa nahodha wake John Terry na mshambuliaji wake Eden
Hazard watakosa mechi ya jumapili na wapo hatarini kuwakosa Atletico jumatano.
0 comments:
Post a Comment