JOSE Mourinho amethibitisha kuwa Peter Cech
atakosa mechi zote zilizosalia msimu huu baada ya kuteguka bega, lakini
amesisitiza kuwa Chelsea inahitaji kufika fainali ili John Terry apate nafasi
ya kucheza tena.
Cech aligongana na Raul Garcia kipindi cha kwanza
katika suluhu ya bila kufungana na Atletico Madrid na alipelekwa moja kwa moja
hospitali kupimwa.
Wakati huo huo, Terry aliumia kifundo cha mguu
baada ya kukanyagwa na Diego Costa katika dakika ya 71.
Nahodha huyo wa Chelsea alijitahidi kuendelea
kucheza lakini alishindwa na kutoka.
“Peter Cech msimu kwake umekwisha” Mourinho amewaambia
waandishi wa habari baada ya mechi.
“Kwa John (Terry), tunatakiwa kucheza fainali ili
acheze tena”.
Terry na Cech watakosa mechi ngumu ya ligi kuu
England dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield jumapili ya wiki hii na
mechi ya marudiano na Atletico aprili 30 mwaka huu darajani.
John Obi Mikel na Frank Lampard watakosa mechi ya
marudiano kufuatia kupata kadi mbili za njano, lakini Branislav Ivanovic atakuwepo baada ya kumaliza adhabu yake ya
kusimamishwa;
0 comments:
Post a Comment