Tuesday, April 22, 2014

359486_heroa
BAADA ya kibarua cha David Moyes kuota nyasi Manchester United, kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amempa pole sana.
Moyes amefanya kazi kwa miezi 10 tu katika mkataba wake wa miaka 6 na kocha mchezaji  Ryan Giggs ametangazwa kuwa kocha wa muda mpaka mwishoni mwa msimu.
Louis van Gaal anapewa nafasi ya kuchukua nafasi hiyo, japokuwa anahusishwa kuhamia Tottenham.
Chaguo la kwanza ni Jurgen Klopp ambaye leo hii imejitoa kuitaka kazi hiyo kwa madai kuwa bado ana kibarua Borussia Dortmund mpaka mwaka 2018.
“Sipendi sana kuzungumzia. Nampa pole sana, ni kawaida’. Mourinho ameiambia ITV.
“Nampa pole David kama ninavyowapa pole makocha wengine wanaopoteza kazi”
Moyes aliyevunja rekodi nyingi za Manchester United kwa muda mfupi aliokaa Old Trafford, amekuwa kocha wa kwanza kutimuliwa tangu ilipotokea hivyo kwa Ron Atkinson  mwaka 1986.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video