ASERNAL imezidi kujiweka katika mazingira mazuri
ya kuingia timu nne bora za ligi kuu soka nchini England msimu huu na kufuzu
kucheza UEFA mwakani baada ya usiku huu kuilaza Newcastle mabao 3-0 kwenye
uwanja wa Emirates.
Mabao ya Laurent Koscielny, Mesut Ozil na Olivier
Giroud yameifanya Asernal iweke pengo la pointi nne dhidi ya wapinzani wao
wakubwa wa nafasi ya nne, klabu ya Everton.
Kwa matokeo hayo, Asernal imefikisha pointi 73
katika nafasi ya nne, huku Everton wakisalia nafasi ya tano kwa pointi 69, na
timu zote zimebakisha mechi mbili mbili kufunga msimu.
Asernal hawakutarajia kama wangekuwa hapo walipo
kufuatia kuanza vizuri ligi kuu msimu huu na walionekana kuchanganyikiwa zaidi baada
ya kufungwa katika uwanja wa Goodison Park.
Wiki tatu baadaye, Everton walianza kuteteleka na Asernal kurudi
katika moto wake baada ya kurejea kwa nyota wake Aaron Ramsey na Mesut Ozil.
Kumaliza katika nafasi ya nne jumlisha kombe la FA
yatakuwa mafanikio kwa kocha Aserne Wenger msimu huu na pengine yatachangia
kumwaga wino katika mkataba mpya wa kuifundisha klabu hiyo.
Asernal wanaweza kujihakikishia nafasi ya nne kama
wataifunga West Bromwich Albion jumapili
ya wiki hii, huku wakisubiri mechi yao ya kufunga msimu dhidi ya Norwich.
0 comments:
Post a Comment