HALI
shwari sasa!. Mshambuliaji wa Manchester United, Mholanzi, Robin Van Persie
ameamua kuendelea kukaa katika klabu hiyo kufuatia kufukuzwa kwa David Moyes.
Kilichomvutia zaidi nyota huyo ni klabu hiyo ya Old
Trafford kutaka kumleta Mholanzi mwenzake, Louis Van Gaal kurithi mikoba ya ukocha
mkuu.
Taarifa
za kuaminika zinaeleza kuwa Van Gaal tayari ameshakubali vipengele vya mkataba saa
48 zilizopita ili kuwa kocha wa kudumu wa Man united.
Sio
siri kuwa Van Persie amekuwa na mahusiano mazuri na kocha wake wa timu ya taifa
na sasa anaona itakuwa jambo zuri kukaa pamoja Old Trafford baada ya kumalizika
kwa fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Taarifa
za ndani ni kuwa kocha huyo wa Uholanzi na nahodha wake RVB wanatumia wakala
mmoja, bwana Kees Vos ambaye kwasasa yupo katika vikao vya makubaliano ya kazi
mpya baina ya Van Gaal na Man United.
Van
Persie alikuwa akihusishwa kuihama Man United majira ya kiangazi mwaka huu
kwasababu klabu yake imeshindwa kufanya vizuri kama ilivyokuwa katika msimu
wake wa kwanza ambao alibeba taji chini ya Sir Alex Ferguson.
Pia
kulikuwa na hali ya kutoelewa na bosi wake David Moyes kwa madai kuwa mbinu za
ufundishaji za Mscotish huyo zilikuwa haziendani na mfumo wa uchezaji wa Van
Persie.
Lakini
nahodha huyo wa zamani wa Asernal ameamua kukaa Man United hata kama klabu
inatarajia kusaka mshambuliaji mwingine wa kati kwa sababu bosi wake anakuja.
0 comments:
Post a Comment