Mchezaji Sylvain Azougoui alifariki uwanjani baada
ya kupiga teke ya kichwani
...............................................
Mchezaji
wa klabu ya Ac Bongoville,Sylvain Azougoui amefariki baada ya kupigwa
teke ya kichwani wakati wa mechi ya ligi kuu nchini Gabon.
Kipa
huyo alifariki alipokuwa akipelekwa hospitalini baada ya tokeo hilo
wakati wa mechi yao dhidi ya klabu ya Centre Mberi Sportif.
Kipa
huyo mwenye umri wa miaka 30 kutoka Togo alikuwa amelisimamisha kombora
lililopigwa langoni mwake, lakini mshambulizi alipoteza mwelekeo na
kumkanyaga Azougoui kichwani.
Mechi hiyo ya siku ya Jumapili ilichezwa Bongoville ambalo liko umbali wa kilomita 800 kutoka Libreville mji mkuu wa Gabon.
"Ni vigumu sana kushuhudia hali hii ya uchungu ,'' ilisema taarifa katika mtandao wa klabu hiyo.
Chanzo: BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment