Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
BONDIA bingwa wa UBO Afrika, Thomas Mashali maarufu
kwa jina la `Simba asiyefugika` amewaasa wanamasumbwi wenzake kufanya mazoezi
muda wote ili kujiimarisha kwa mapambano.
Mashali ameueleza mtandao huu kuwa hakuna uchawi wa
kufanikiwa katika mchezo wa ngumi zaidi ya kujikita katika mazoezi ya kijiweka
sawa muda wote.
“Mabondia tuna tabia ya kujisahau hasa pale tunapopata
mafanikio. Wenzetu wa nchini hawana masihara kabisa”.
“Wanatambua kuwa ngumi ni ajira yao kama ilivyo
kwa kazi yoyote, muda mwingi wanatumia katika mazoezi”.
“Lakini sisi tunaleta mchezo na ndio maana
tukikutana nao tunashindwa kutamba”. Alisema Mashali.
Simba asiyefugika alisema kwa upande wake
anajitahidi kufanya mazoezi katika `jimu` ya `Lazima ukae Gym` inayomilikiwa na
mdau wa ngumi, Mawzo Njenje.
“”Namshukuru sana Mawazo na Gym yake ya `Lazima
Ukae`. Nimekuwa nikikutana na wenzangu kama akina Francis Miyeyusho kuhakikisha
tunajiweka sawasawa. Nafahamu kuwa mazoezi ndio uchawi wangu”. Aliongeza
Mashali.
Aidha, Mashali aliwataka watu wote wanaopenda
Masumbwi kuwa wazalendo na waungwana katika utaoaji wa zawadi katika mapambano.
“Mimi nashangaa sana niliopokuwa napigana na
Japhet Kaseba mwezi uliopita kuwania ubingwa wa UBO Afrika. Kuna jamaa aliahidi
Gari kama Kaseba atashinda, lakini nikishinda mie anaondoka na gari yake”.
“Huu si uanamichezo. Gari ingeahidiwa kwa yeyote
atakayeshinda. Kumuahidi mmoja ni ubaguzi na inaonesha kutokomaa katika michezo.
Narudia watu kama hawa si mwanamichezo”. Alisisitiza Mashali.
Pia aliitaka serikali kupitia wizara yenye dhamana
kusimamia michezo kuhakikisha inawasaidia mabondi wake hasa katika mapambano ya
kimataifa.
“Kuna wakati nilikuwa Afrika kusini, nikapigiwa
simu kuwa Mashali njoo Tanzania kuna pambano nchini Urusi. Nilipofika Tanzania
nikaambiwa na rais wangu wa PST Emmanuel Mlundwa kuwa ninaenda Urusi kucheza pambano lisilo na
ubingwa, raundi 8”
“Nikamwabia dola ngapi? Akaniambia nikakubali.
Nikapatiwa mikataba na kusaini. Nafika Urusi nakumbana na hali tofauti”
“Naambiwa nacheza pambano la ubingwa, tena wa
dunia raundi 12. Nimuuliza Mlundwa vipi? Anasema na yeye haelewi. Nilipoteza
mchezo”
“Niliumia sana kwasababu ningeambiwa mapema
ningejiandaa vizuri. Kuna usanii mwingi unafanyika tunapoenda nje, serikali
itusaidie mabondia” Alisema Mashali.
0 comments:
Post a Comment